512; Mimi Ni Mtenda Dhambi Kuliko Wewe.

Siku Moja nilikuwa nawaza hivi, “Siku Nikifa Nikakuta hakuna Mungu Nitacheka Sana”, Sauti nyingine ndani yako Ikasema, “Hapo Utakapokuwa Unachekea ni Nani Huyo Atakuwa Amekutengenezea” Ndugu Yangu Mungu Yupo, Ukatae Ukubali………………… Kuna ule mtazamo wa kuwaona watu ambao wamefanya mambo makubwa, na wale wenye ushawishi mkubwa sana kuwa hao ni watu wasio na makossa kabisa.…

489; Hizi Ndio Fikra Zinazokufanya Usiendelee Kwenye Maisha.

Ndani ya jiji lenye watu wengi kuliko miji mingine ndani ya Tanzania jiji la Dar es Salaam, kumekuwa na changamoto kubwa sana ya Usafiri. Hivyo basi serikali pamoja na watu binafsi wamekuwa wakiwaza kila siku ni njia gani inaweza kuwa suluhisho la tatizo hili. Katika kufikiri huko kukatokea watu wawili ambao walikerwa sana tatizo hili…

SURA YA 440: Usichanganye na Maji.

Miaka kama 10 iliyopita Kulikuwa na bibi mmoja kijijini kwetu alikuwa anauza maziwa fresh. Maziwa yake yalikuwa ni matamu sana na pia masafi hivyo kusababisha watu wengi kuyapenda na kuyasemea vizuri. Kadiri watu walivyoyasemea vizuri ilifika wale waliokuwa wanauza maziwa kama yeye ikabidi wafunge kwa kukosa wateja. Watu Karibu mtaa mzima ulihamia kwake. Bibi yule…

SURA YA 428; Ukitegemea Hiki Pekee Utachoka Haraka.

Mwanadamu pekee aliekuwa na akili sana kuliko wanadamu wengine ni Adamu na yeye alipewa uwezo huo kwasababu alikuwa peke yake. Hivyo kwa akili na uwezo aliokuwa nao ukamuwezesha kuyaendesha Maisha yake kwa urahisi. Kwasasa kila unachotaka kukifanya kwa kiasi kikubwa kinategemea wengine, inawezekana ni vifaa, au hata watu wengine utawahitaji ili uweze kuwa na ufanisi…

SURA YA 427; Njia Rahisi ya Kuwavuta Watu Sahihi Kwako.

Tupo kwenye dunia ambayo ni ngumu sana kumjua mtu kwasababu wengi wamevaa mavazi yanayofunika uhalisia wao. Wamevaa tabia za kuigiza ambazo sio za kweli na wala hawana kabisa. Wamevaa Maisha ambayo ni uongo na ndani yake wanateseka huku wakifurahia kuona watu wanawasifia. Sasa ili uweze kuwavuta watu sahihi na kuwaacha hawa waliojivalisha mavazi ya uongo…

Subscribe