Umekutana na mtu ukatamani sana kuzungumza nae lakini ghafla yakaanza kuja mawazo kichwani kwako kwamba, “huyu atakuwa anaringa” “mimi sistahili” “nitaongea nae siku nyingine”. Mwishoe unaondoka huku ukiwa hujaweza kuzungumza neno lolote. Huu ni woga na hofu ambayo umejitengenezea mwenyewe. Kwanza unatakiwa ujue hata kama hayo unayowaza ni ya kweli basi yeye ndie ana matatizo…
398: Kuwa Mkweli Kwako Kwanza.
Unaweza kuwadanganya wengine lakini huwezi kujidanganya wewe mwenyewe. Ndani ya nafsi yako unajua ukweli ni upi. Ndani ya nafsi yako unajua kama Maisha unaigiza au ni kweli kile ambacho unakionesha. Mojawapo ya vitu vinavyowatesa wengi ni kujaribu kujidanganya wenyewe, unakuta unajua kabisa Matendo yako hayaashirii kabisa kile ambacho unataka lakini unajitia moyo wa uongo kwamba…
397: Jinsi ya Kuondoa Imani Potofu Ambazo Ulijengewa Ukiwa Mtoto.
Mtu anatengenezwa katika umri wa kuzaliwa mpaka anapokuwa na miaka 7. Tabia Nyingi na Imani ambazo unazo sasa zilijengwa ulipokuwa mtoto. Na mara Nyingi Imani hizi zilijengwa ulipokuwa unaona kile ambacho watu wa karibu na wewe wanafanya. Mtoto anapozaliwa ubongo wake wa kumbukumbu unakuwa mtupu kabisa. Hivyo kila ambacho anaona kinafanyika kinaingizwa kwenye ubongo wa…
HATUA YA 396: Usifanye kwa Kwa Ajili Yako.
Penda kuwaweka wengine mbele kwanza ndio utaweza kufurahia kile unachokifanya. Unataka kununua gari, Sema napambana ninunue gari ili niwahamasishe wengine kuwa inawezekana ” Chochote kile unachokifanya hata kama ni wewe unafaidi jaribu kuweka katika namna ambayo wengine wanaguswa pia. Furaha ya kweli haipo katika vitu tunavyomiliki ila katika watu tunaowasaidia. Furaha ya kweli ipo katika…
HATUA YA 395: Upo Tayari Kufanya Hata Kama Hujisiikii Kufanya?
Watu waliofanikiwa wanaendelea kufanikiwa kwasababu wapo tayari kufanya hata yale ambayo hawajisikii kufanya. Unajua kuna vitu unatakiwa kuvifanya halafu mwili unakuwa umechoka hivi unasema nitafanya kesho au siku nyingine. Kuna wakati unakuwa umechoka sana hadi yale mambo ya muhimu unataka kuahirisha, unatakiwa ujue kwamba kitu pekee ambacho hutakaa ukipate tena ni muda. Lazima ukubali kujitoa…
HATUA YA 394: Kama Hutengenezi Maadui….
Ni kweli hutakiwi kufanya kutafuta maadui kwasababu haina maana yeyote, ila katika safari ya mafanikio huwezi kuepuka kuwa na maadui. Kuna watu watakuchukia tu bila sababu yeyote. Wengine watakuchukia kwasababu kile unachokifanya wao hawajaweza kufanya, wengine watakuchukia kwasababu wameona umeanza kuwapita kwasababu mnafanya kitu kinachofanana. Sasa wakati mwingine ili kujua kama kweli unasonga mbele na…
HATUA YA 393: Yeyote Anaejaribu Kukuzuia…
Ukiona kuna mtu ana muda mwingi sana wa kufuatilia unachokifanya na siku zote anakuja na mawazo hasi tu na wala hujamwajiri afanye hivyo basi ujue tu huyu Ameshapoteza Muelekeo wa Maisha Yake Mwenyewe. Huo ndio ukweli kama yeye Maisha yake hana muda nayo ndio anapata muda wa kufuatilia Maisha yako maana yake yeye ameshayapoteza Maisha…
HATUA YA 392: Una Uwezo wa Kudhibiti.
Imekuwa ni kawaida kusikia watu wanalalamika wameumizwa kihisia, na wanasema hawatakaa wapende tena. Imekuwa ni kawaida pia kuona watu wakilalamikia mambo mbalimbali ambayo walijitoa sana na kisha yakaja kuwaumiza kuliko walivyotarajia. Unachotakiwa kujifunza hapa ni wewe binafsi kujitahidi uweze kudhibiti hisia zako. Usipende kuziachia zikatoka au zikaonekana san ahata kwa mtu ambaye bado hujajua kama…