NGUVU MPYA 419; Inuka hapo, Kuna Mwingine Ana Zito Zaidi Ya Lako.

Mahali ulipo sasa hivi na hayo unayopitia unaweza kuyaona ni magumu sana. Unaweza kufikia hatua ya kujutia hata kwanini ulizaliwa kwasababu unajiona kama wewe pekee ndie mwenye mateso na majaribu makubwa sana duniani. Ukweli ni kwamba hayo unayopitia ni majaribu kweli ni magumu pia. Ila kwasababu hapo ndio sehemu uliyofika ndio maana unayaona kama ni…

418; Fanya Kitu Hiki Muhimu Siku Chache Zilizobakia Mwaka Huu.

Pamoja na kwamba inawezekana unaona kama mwaka huu mambo hayajaenda sawa kabisa na malengo mengi hayajatimia bado una nafasi ya kumaliza mwaka vizuri sana. Kuna mambo machache tu ukiamua kuyafanya kwa siku hizi zilizobaki baki unaweza kupata furaha kubwa sana ndani ya moyo na ukajisikia utoshelevu. Watazame wale ambao unawapenda inawezekana ni mwenzi wako, Watoto,…

417; Ukianzia Juu Utashuka Chini.

Mojawapo ya vitu ambavyo huanza juu havipendezi sana na sio vizuri mfano wa haraka ni shimo. Shimo linachimbwa kwa kuanzia juu kwenda chini na shimo linaweza kuwa hatari lakini vitu vingi vizuri huanzia chini na kuelekea juu. Unapojenga ghorofa lazima uanze chini kuweka msingi ndio upande juu Zaidi. Sasa Rafiki ukitaka usiteseke, kwasababu wengi wanateseka…

416; Huwezi Kujua Kama Wewe Ni Jasiri Bila Hiki.

  Ukikutana na watu wawili wanagombana na mmoja anasema ntakupiga,ntakuumiza halafu hafanyi chochote bali anaendelea kusema t umara nyingi mtu huyo huwa ni mwoga. Mwoga hutishia kwa maneno mengi kwamba anaweza hiki anaweza kile lakini jasiri huacha kusema naweza hiki bali huonesha pale panapotakiwa kuoneshwa. Sasa kama wewe upo kwenye uwanja wa mapambano hutakiwi kusema…

415; Huwezi Kuwa Kamili Jikubali Ulivyo.

Siku zote kama unaishi na watu ambao unaona kama wamekuzidi vitu vingi, utakuwa unajiona wewe ndio hujakamilika. Unaweza kuona wengine wanavaa vizuri kuliko wewe, wanakula vizuri kuliko wewe, wanaendesha magari mazuri kuliko wewe, wana wenza wazuri kuliko wewe. Hii inasababishwa na wewe kujisahau kabisa na kutoangalia vile vizuri ambavyo umebarikiwa. Kama utatumia muda mwingi kutazama…

414; Hujachagua Kuzaliwa, Hujui Utakufa Lini, Unaweza Kimoja Tu.

Maisha ni ya ajabu sana, unazaliwa bila idhini yako mwenyewe, pengine hata wazazi wako hawakutarajia wala kupanga wewe uzaliwe. Na hata kama wakipanga hawawezi kujua kabisa ni mtu wa aina gani anazaliwa, vipimo vinaweza kujua jinsia lakini haviwezi kujua ile jinsia imebeba mtu wa namna gani. Kingine cha ajabu sana sasa ni kuwa hujui utakufa…