499; Njoo Uchukue Milioni Kesho.

Ikitokea Rais amesema vijana wote kesho tukutane nae pale Posta Dar es Salaam Atakuwa anagawa Tsh 1m ukafanyie chochote unachotaka, popote ulipo bila kujali unafanya nini bado nafasi ya kwenda utaipata. Huwezi kusema samahani naomba nije kuchukua keshokutwa, huwezi sema nitakuja jioni naomba unisubiri, huwezi kusema umepata dharura akutumie kwa mpesa. Utakachokifanya ni kwenda na…

498; Huwezi Kunizuia Tena.

Unajua hakuna kisichowezekana kwenye dunia hii endapo utakuwa umeweka nia ya dhati ya kutaka kufanikisha. Endapo utaamua kwamba hakuna chochote kinachoweza kukuzuia tena, ukikubali kila kitakachokuja mbele yako kiwe kibaya au kizuri utaamua kukitumia kama silaha ya kukusogeza mbele. Nikuambie kitu mimi sijazaliwa kwenye familia yenye nafuu ya aina yeyote, nimewahi kukosa ada ya shule,…

495; Toka Kwenye Maboksi Ya Wengine.

Kuna vile unajihisi wewe haupo sawa kisa tu maisha yako hayafanani na ya fulani. Elimu yako haiendani na watu fulani, huna cheo cha maana kwenye kazi. Naomba nikwambie hayo yote ni maboksi watu waliojitengenezea Usikubali kuishi kwenye maboksi ya wengine Tengeneza boksi lako linalokutosha. Sio lazima uwe na elimu kubwa kama wengine, sio lazima uwe…

494; Endapo Maisha Yote Uliyoishi Mpaka Sasa Yangekuwa ni Ndoto.

Habari Rafiki, leo naomba ujiulize swali hili la msingi sana. Iwapo umeamka asubuhi halafu ukajitazama ukakuta umerudi nyuma miaka 10 au ishirini iliyopita. Yaani kumbe yote yaliyotokea kwenye Maisha yako miaka kumi iliyopita ilikuwa ni ndoto tu ulikuwa unaota usiku wa jana. Swali la msingi la kujiuliza je hiyo ndoto itakuwa inatamanisha kuwa kweli? Je…

Jacob Mushi

Afya, Hekima na Utajiri

Skip to content ↓