Mama anapobeba ujauzito kwa kawaida inajulikana kwamba ni baada ya miezi 9 ndipo mtoto huzaliwa. Kadiri muda unavyokwenda kuisogelea ule mwezi wa 9 ndipo shauku huwa kubwa juu ya kupokea mtoto. Kitakachowafanya wawe na nguvu kubwa Zaidi ya kufurahia mtoto ajaye ni pale daktarin anaposema mtoto atazaliwa tarehe 25 au 26. Vile vile kwenye Ndoto…
HATUA YA 355: Epuka Ugonjwa wa Kutaka Kuwa Sahihi/Kutaka Kueleweka na kila mtu.
Umeshawahi kujikuta unafanya kitu kimoja na hukimalizi kwasababu kila ukikitazama unakiona kama hakijakamilika bado? Umeshakutana na hali ya kutaka kila kitu kiwe kiko sawa ndio uanze kuchukua Hatua? Umepata wazo la kuanzisha biashara unaanza kuogopa “nikianza kabla sijaitengeneza vizuri sana ninaweza nikashindwa.” Au huu wimbo naona bado haujanivutia sana ngoja nirudi studio tena, au hichi…
HATUA YA 354: Usijipe Tafsiri ya Mabaya.
Unaweza kupitia hali mbaya muda mrefu kwenye Maisha yako hadi ukaanza kujiona wewe ni yule mtu ambaye anapitia hali mbaya. Unaweza kuwa umeshindwa kudumu kwenye mahusiano na watu mbalimbali kiasi kwamba ukaanza kujiona wewe ndio uko hivyo yaani wewe haukaagi kwenye mahusiano muda mrefu. Inawezekana pia hadi sasa umeshafanya biashara nyingi na zote zimefeli yaani…
HATUA YA 353: Uko Vile Ambavyo Unajiona.
Haijalishi sana watu wanasema au wanajua wewe ni nani kuliko vile ambavyo wewe binafsi ndani yako unavyoamini. Wapo wengi wanaweza kukusifia au kukuona hufai kama wewe binafsi utakuwa hujioni unafaa yote hayo hayatasaidia. Unapaswa kutengeneza yule mtu ambaye unataka kuwa, andika vile ambavyo unajiona katika mtazamo chanya. Vile ambavyo ungejisikia vizuri Zaidi ukiwa hivyo. Imani…
HATUA YA 352: Unachokikwepa Sasa Hivi…
Kiumbe hai chochote kina Hatua mbalimbali za ukuaji ambazo kinapitia hadi kufikia sehemu ambayo inakuwa ni ya ukomavu. Ili kiumbe hiki kije kuwa na mwisho mzuri lazima Hatua hizi zifuatwe kwa utaratibu. Huwezi kusema umepanda mahindi leo na ukayawekea mbolea na dawa le oleo ili yakue kwa haraka. Ukikimbilia kuyawekea mbolea mapema au ukayanyeshea maji…
HATUA YA 351: Ukianza Kuona Una Sababu Nyingi…
Mwanadamu siku zote hapendi aonekane anahusika na makossa yake mwenyewe. Na inapotokea amekosea au ameshindwa jambo Fulani anatafuta mtu wa kumbebesha yale makossa yake. Tangu mwanzo wa kuumbwa kwa dunia tunaona Adamu na Hawa walipopatikana na kosa la kula tunda la mti walioagizwa wasile kila mmoja alianza kutoa sababu za kwanini alifanya vile. Adamu ambaye…
HATUA YA 350: Kama una Imani ya Aina Hii Utapata Tabu Sana.
Imani huja kwa kusikia, tunasikia vitu vingi sana tunavyovihitaji na tusivyovihitaji kabisa kwenye maisha yetu. Kile unachokipa nafasi ya kukisikia zaidi kinajenga imani ndani yako. Kama unafuatilia kufanikiwa, unasikiliza na kusoma mafundisho ya mafanikio unajenga imani katika Mafanikio. Kama utawekeza muda wako katika kufuatilia bahati nasibu, kubeti, kufanikiwa kwa ghafla na imani yako itajengwa huko.…
KANUNI YA 10× INAVYOWEZA KUKUFANIKISHA KWENYE MAONO YAKO.
Unafahamu pamoja na kuwajua watu wengi sana katika Maisha yako kuna watu angalau 10 tu ambao wanaweza kuwa tayari kukuinua pale unapokuwa umeanguka chini? Mtu wa kawaida kabisa ana watu wake wa karibu 10 ambao wapo tayari kununua au kuchangia kila anachokifanya. Ukweli ni kwamba hawa kumi wanaweza wasitoshe kununua bidhaa yako au kulipia huduma…