Kwanza nataka ujijengee mtazamo huu kwenye akili yako, tatizo lolote linapotokea kwenye Maisha yako usiwe mwepesi sana kuona wengine ndio wanahusika, anza kuona wewe umehusikaje, imekuaje ukawa katikati ya tatizo hilo. Kuwepo katikati ya tatizo ina maanisha kuna mahali wewe ulikosea hadi ukafika hapo. Ukisalitiwa inamaanisha kuna mahali ulikosea ukajikuta uko kwenye kusalitiwa, ndio unaweza…
All posts in MAFANIKIO MAKUBWA
483; Unapohisi Kama Mungu Amekuacha
Kumzuia mtoto asitembee mwenyewe kwasababu tu unaogopa ataanguka na ataumia sio kumsaidia ni kumlemaza. Hivyo ndivyo ilivyo katika maisha yetu ya kila siku. Kuna vitu kama utaendelea Kuogopa kufanya au kutaka Kusaidiwa kila unapofanya unakuwa unalemaa. Lazima ujifunze kufanya mwenyewe ili uwe na Ujasiri na kujiamini. Kamwe usifikiri Mungu amekuacha wakati wa magumu anataka ujifunze…
482; Mbegu Inayojiotea Yenyewe.
Mti unapopukutisha majani na matunda unaweza kufikiri imepoteza kitu kikubwa sana. Mfano ndege wanapokuja na kula matunda kisha yakaanguka chini yakaoza. Wewe kwa akili zako za kibinadamu unaweza kuona ni uharibifu. Lakini kwa akili za Kimungu sio uharibifu yale matunda yaliyooza hugeuka kuwa mbolea kwa mti ule ule ulioyadondosha. Kuna vitu ukivifanya kwenye Maisha ya…
480; Tambua Kusudi La Mungu Maishani Mwako.
Unaweza kujikuta unafanya mambo hayaendi kabisa na wala huoni matokeo yake unayoyataka kwasababu upo nje ya kusudi la Mungu. Mungu hajakuumba kwa bahati mbaya ulikuja kwa kusudi na upo hai ili utimize kusudi. Hakikisha unalitambua kusudi la Mungu maishani mwako ili uweze kuishi maisha yenye furaha na baraka za Mungu. Hujazaliwa duniani ili uje kuzaa…
479; Kabla Hujakata Tamaa, Jaribu Njia Nyingine.
Kuna Wakati wale uliowatarajia Wakusaidie watakugeuzia Mgongo. Usiogope, Usilaumu, Usilalamike Mtumaini Mungu, na Jaribu Njia Nyingine. Mwaka 2016 nilijitoa muhanga wa kutafuta mtaji wa kufanyia biashara. Niliingia kwenye simu yangu nikaona nina namba zisizopungua elfu moja. Katika hizo namba watu Karibu 500 walikuwa wananifahamu. Nikasema ngoja niwatumie watu hawa kukusanya mtaji. Nikaandaa ujumbe mzuri nikawatumia…
472; Mbinu za Kuweza Kuwa na Furaha Wakati Wote.
Kuna utafiti ulifanyika wa kidunia ukaja na majibu ya nchi zinazoongoza kwa kukosa furaha duniani. Mojawapo ya nchi iliyotajwa ilikuwa ni nchi ya Tanzania, kwasababu mimi ni mtanzania sikuwa na majibu sahihi wala utafiti wa kupinga hili ila ninaweza kukuandikia wewe mambo machache ambayo unaweza kufanya na yakakuletea furaha binafsi. Watu wengi wamekuwa wanafikiri kwamba,…