404; Ni Wachache Sana Wanaweza Kujibu Swali Hili.

Ukimuuliza mtu akutajie mambo 3 ya muhimu sana kwenye Maisha yake ni wachache wataweza kukujibu kwa usahihi nikiwa na maana kwamba walikuwa wanayajua kabla hujawauliza. Ni rahisi mtu kujibu kwa kutamka kile ambacho kitamjia kichwani kwa wakati huo lakini ukweli ni kwamba utakuta hafanyi chochote katika hayo aliyosema ni ya muhimu kwenye Maisha yake. Embu…

403; Maneno Yao Sio Uhalisia Wako.

Wanaweza Kusema yule jamaa alifeli shule hajaweza kufika hata chuo hawezi chochote. Wanaweza kusema yule dada kila mahusiano yamemshinda hawezi kutulia na mwanaume. Wanaweza kusema pia pombe zitakuja kukuua siku moja. Wanaweza kusema wewe ni mtu wa maneno maneno sana na huwa unaongea vitu visivyoeleweka. Hayo yote na mengine ambayo wanaweza kusema juu yako ni…

402; Mtu Huyu Anakudanganya.

Ulishawahi kutaka kukutana na mtu akakujibu kwamba hana muda? Umewahi kujiuliza ni kwanini anasema hana muda? Je kuna ukweli wowote pale anapokwambia hana muda? Wanadamu wote tumepewa masaa 24 kila siku na hii ni mojawapo ya vitu ambavyo kila mmoja anacho kwa usawa kabisa. Kinachotutofautisha ni yale ambayo tunatumia kwenye muda wetu kila siku. Kuna…

401; Kila Kitu Kilianza Kama Wazo.

Tangu mwanzo wa kuumbwa kwa ulimwegu huu kila kitu kilianza kama wazo. Mungu alikaa akawaza kuleta uhai katika sayari ya dunia baada ya sayari hii kuwa imejaa maji pekee yake. “Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu” (Mwanzo 1:26). Na hakuishia hapo vitu vingine vyote ambavyo unaviona havikutokea tu vyenyewe bali vilitokana na mawazo yake mwenyewe. Kitu…

Ni wewe Mwenyewe Umechagua 18/11/2018.

“Mwaka 2016 tulikuwa kwenye msiba wa jirani yetu ambaye alifiwa na mama yake. Siku hiyo watu walikuwa wanalia sana na kusikitika kwa kifo kile kilichotokea. Kitu kimoja ambacho kilimshangaza kila mtu ni kwamba mtoto wa kiume wa marehemu alikuwa hana machozi na wala hana huzuni sana kama ambavyo wengi walidhani itakuwa hivyo. Watu wakajikuta wanajiuliza…

VITU 5 UNAVYOPASWA KUVIFAHAMU ILI UWEZE KWENDA NA KASI YA MABADILIKO-9/11/2018

Tupo kwenye dunia ambayo kila kukicha kunakuwa na mabadiliko mapya katika sehemu mbalimbali hasa za kiteknolojia. Kama mwanadamu ukishindwa kwenda na kasi hii kuna mambo mengi utajikuta unashindwa kufanya au unalipa gharama kubwa sana ili tu yafanyike. Kuna vitu vingi ambavyo ungevijua vingeweza kuwa rahisi sana kwako kugundua fursa mbalimbali ambazo zingekuingizia kipato. Kwasababu hujafahamu…