Ulishawahi kwenda mahali ukapotea njia? Unajua ni faida gani unapata baada ya kupotea njia? Kwanza unakuwa umejua njia nyingine ambayo haiendi kule ulipokuwa unakwenda. Pili utakuwa umegundua njia ambayo itakufikisha kule ulipokuwa unataka kwenda kwasababu ulipopotea uliuliza kisha ukaelekezwa. Sasa kama wewe ulikuwa hujui kule ulipokuwa unakwenda na ukaweza kwenda bila ya kupotea kuna hatari…
All posts in HATUA ZA MAFANIKIO
HATUA YA 315: Hiki Ndio Kipimo cha Thamani ya Unachokifanya.
Lipo swali moja ambalo unapaswa kujiuliza kila wakati kwenye kile ambacho unakifanya kila siku. Inaweza kuwa ni kazi yako, kipaji, biashara au chochote kile kinachokuhusisha wewe na watu. Ni jambo jema sana kujua maendeleo yako na kama kweli unachokifanya kinaongeza thamani kwa wengine. Lazima ujiulize, Hivi nikiacha leo kufanya hiki kitu Itakuaje? Kama ni ajira;…
HATUA YA 314: Unaamini Nini?
Imani ndio inaweza kuamua matendo ya mtu juu ya kile unachokifanya. Huwezi kufanya jambo kwa ujasiri na kujiamini kama huna imani nalo. Imani inazidi uwezo ulio nao. Unaweza kuwa na uwezo mkubwa sana lakini kama huna imani ya kufanikiwa kwenye jambo unalolifanya utajikuta unashindwa kila wakati. Kuna vitu vingine unashindwa sio kwasababu hujui au una…
HATUA YA 313: Historia Itakuhukumu.
Kuna mambo ambayo tunafanya sasa wakai mwingine tunaweza kuwa tunabishana sana juu ya nani yupo sahihi na nani amekosea. Ukweli unaweza usielewe kwa haraka kwasababu wengi wanaweza kutumia mapenzi binafsi na kuangalia kile wanachokipata kwa wakati huo. Mambo mengine yakiwa magumu katika kuujua ukweli tunaachia muda kadiri muda unavyokwenda ndio tutajua nani alikuwa mkweli na…
HATUA YA 312: Njia Rahisi Zaidi.
Kuna wakati mtu anaweza kuja kuomba ushauri halafu akategemea kwamba utampa njia rahisi Zaidi au shortcut ya kutatua changamoto zake. Wakati mwingine unaweza ukapewa njia ngumu Zaidi lakini yenye manufaa kwako wewe mwenyewe. Kutegemea kupewa njia rahisi ndio kunawafanya wengi waache kufanya vitu sahihi na mwishoe kupotea. Kama utategemea upewe muujiza wa kutatua changamoto yako…
HATUA YA 311: Mtazamo wa Kuwa Juu Wengine Chini.
Huwezi kuishi kwa furaha na Amani duniani kama una mtazamo wa kuwakandamiza wengine ili wewe uonekane upo juu. Kuna mtazamo ambao wengi wanao na wamekuwa wakiamini kwamba ili uwe juu lazima wengine wawe chini. Ili uwe Tajiri lazima wengine wawe maskini, ili uwe na nguvu lazima wengine wawe dhaifu, ili uwe na umaarufu lazima wengine…