“Ilikuwa ni siku za mwisho wa mwaka ambapo tulikuwa na utaratibu wa kwenda kuwasalimia ndugu na jamaa ambao hatujawaona miaka mingi. Katika kuwatembelea ndugu jamaa na marafiki wengi siku moja nikapitia kwa ndugu mmoja ambaye hatukuonana muda mrefu sana. Huyu ndugu baada ya kunipokea alinisisitiza sana nile chakula. Nilimkatalia kwasababu nimepita nyumba nyingi na nimeshakula.…