Leo nataka ujiulize kwanini Mungu alikuumba wewe mwanadamu na wala sio kiumbe kingine chochote? Ukijua hivyo huwezi kujidharau! Ukijua hivyo huwezi kujifananisha na wengine! Ukijua hivyo huwezi kukubali kushindwa! Ukijua hivyo huwezi kukata tamaa kirahisi! Utajua unapoelekea! Utajua watu wakuambatana nao! Utajua ni vitu gani vya Kusoma! Mnyama wa kawaida hua anawaza vitu viwili tu…
JINSI YA KUANZIA CHINI KABISA NA BIASHARA YAKO
Habari za leo Ndugu. Unaendeleaje na katika kutafuta Maisha ya mafanikio? Leo nimekuletea mada nyingine ya muhimu sana baada ya mada ya mada ya mtaji. Haya mambo mazuri tunayozungumza hapa njia nzuri ya kupata matokeo ni kufanyia kazi haya unayojifunza bila kukata tamaa. Haijalishi utakutana na changamoto kiasi gani unatakiwa uendelee kupambana uzivuke ili ufikie…
HATUA YA 23: Unataka kwenda Mbali au Unataka Kufika Haraka?
Kuna msemo mmoja unasema kwamba “Kama unataka kufika haraka nenda/tembea mwenyewe. Kama unataka kufika mbali usiende peke yako nenda pamoja na wengine. “If you want to go quickly, go alone. If you want to go far, go together.” Ukienda peke yako Hutafika mbali, hutaenda mwendo mrefu utachoka. Kama safari yako ni ndefu usichague kwenda peke…
HATUA YA 22: Unacho cha Kupoteza?
Katika Maisha kuna mambo mengi sana huwa yanajitokeza na yanatufanya tuwe na hali za furaha au wakati mwingine hasira. Juzi wakati nasafiri kwenda Mwanza, kwenye bus kulikuwa na mtu alilipa akaa kwenye siti mbele ya safari akaja kuambiwa ilikuwa na mtu tayari yupo kituo cha mbele hivyo asimame. Pale ndani ya gari kukatokea mabishano makubwa…
HATUA YA 46: Ukweli Utakuweka Huru.
Kuna msemo mmoja unasema ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu. Walisema hivi kwa sababu ukidanganya halafu ukasahau ulichodanganya huwezi kuwa huru. Ukidanganya mara ya kwanza itakubidi udanganye mara ya pili. Uongo ni tabia mbaya sana ndio maana ulipokuwa mdogo ulichapwa sana pale ulipodanganya. Ukweli Utakuweka Huru kwa sababu huna haja ya kukumbuka ulichokisema. Mara zote unapokuwa…
HATUA YA 21: Tafuta Muda Mzuri na Wewe Peke Yako.
Ni Mara ngapi umekuwa ukiwapa watu muda wako? Ni mara ngapi umekuwa ukivipa vitu vya namna mbalimbali kwenye Maisha yako? Umekuwa ukitumia muda mwingi na Tv au marafiki lakini ukasahau kutumia muda na wewe mwenyewe. Umekuwa unatumia muda mwingi kazini kwako na kwenye shughuli zako nyingine lakini hupati nafasi ya kukaa na wewe pekee…
HATUA YA 3 : Hapo Ulipo Sasa.
Hapo ulipo sasa usipadharau na kujiona upo nyuma sana. Kuna wengi sana wanatamani wafikie HATUA uliyofikia wewe. Kuna wengi wanajifunza kwa HATUA uliyofikia leo. Hata kama huoni wanaokupongeza kuna watu wanajifunza mno juu ya kile unachokifanya. Ninasema hivi Kwasababu inawezekana umekata tamaa na kujiona uko chini na wakati Mwingine kutokujali kile ulichonacho sasa. Kijali sana…
HATUA YA 20: Andika Historia.
Kila hatua unayopita hakikisha huachi hivi hivi, Hakikisha uneacha alama. Ni changamoto unapitia Hakikisha haikuachi hivi bure, utoke na cha kujifunza, Hakikisha Unatoka na hadithi Nzuri ya kuwaeleza watu. Maisha yetu yamefungwa kwenye muda, kadiri tunavyotumia muda ndio tunavyomaliza kuishi. Kila unachokifanya Hakikisha kinaacha alama. Watu unaokutana nao Hakikisha unawaacha wakiwa wa tofauti. Hakikisha unawaachia kitu…