Leo nakumbuka siku yangu ya kuzaliwa, nimetimiza miaka kadhaa hapa duniani. Katika kutafakari mambo mbalimbali na kujiuliza maswali nilijikuta katika mawazo haya, “Mimi sijawahi kumuomba Mungu aniumbe binadamu, sasa inakuaje nikikosea ameahidi adhabu mbalimbali?” kwanini niadhibiwe kwa Maisha ambayo hata sijayachagua kuishi? Ukweli ukitafakari hayo maneno yako kama yana ukweli Fulani ndani yake. Lakini hupaswi…
484; Ukiachwa Ni Nani Anakuwa Amepoteza?
Nilimpenda sana, nilimwonesha mapenzi yote, nilimpa kila alichokuwa anataka lakini nimeambulia kuachwa. Hayo ni mojawapo ya maneno ambayo watu wengi wamekuwa wakiyatoa baada ya kuchwa na wale waliokuwa wanawapenda sana. Nimetafakari nikajakugundua kama ni kweli ulikuwa unamfanyia mambo yote mazuri na kumpa kila alichokuwa anataka halafu akaja akakubwaga ukweli ni kwamba sio wewe uliepoteza bali…
483; Unapohisi Kama Mungu Amekuacha
Kumzuia mtoto asitembee mwenyewe kwasababu tu unaogopa ataanguka na ataumia sio kumsaidia ni kumlemaza. Hivyo ndivyo ilivyo katika maisha yetu ya kila siku. Kuna vitu kama utaendelea Kuogopa kufanya au kutaka Kusaidiwa kila unapofanya unakuwa unalemaa. Lazima ujifunze kufanya mwenyewe ili uwe na Ujasiri na kujiamini. Kamwe usifikiri Mungu amekuacha wakati wa magumu anataka ujifunze…
482; Mbegu Inayojiotea Yenyewe.
Mti unapopukutisha majani na matunda unaweza kufikiri imepoteza kitu kikubwa sana. Mfano ndege wanapokuja na kula matunda kisha yakaanguka chini yakaoza. Wewe kwa akili zako za kibinadamu unaweza kuona ni uharibifu. Lakini kwa akili za Kimungu sio uharibifu yale matunda yaliyooza hugeuka kuwa mbolea kwa mti ule ule ulioyadondosha. Kuna vitu ukivifanya kwenye Maisha ya…
481; Fahamu Kanuni za Maisha Bora.
Kila kitu kina misingi na kanuni zake, maisha nayo yana misingi na kanuni zake. Ili uweze kuishi na kufurahia maisha katika kiwango cha juu unatakiwa kufahamu na kuishi misingi na kanuni. Hizi ni ambazo nimezifanya ziwe kama mwongozo wako. AFYA: Afya ya Mwili. Afya ya Akili. Afya ya Kiroho. Vitu Hivi vitatu ni muhimu sana…
480; Tambua Kusudi La Mungu Maishani Mwako.
Unaweza kujikuta unafanya mambo hayaendi kabisa na wala huoni matokeo yake unayoyataka kwasababu upo nje ya kusudi la Mungu. Mungu hajakuumba kwa bahati mbaya ulikuja kwa kusudi na upo hai ili utimize kusudi. Hakikisha unalitambua kusudi la Mungu maishani mwako ili uweze kuishi maisha yenye furaha na baraka za Mungu. Hujazaliwa duniani ili uje kuzaa…
479; Kabla Hujakata Tamaa, Jaribu Njia Nyingine.
Kuna Wakati wale uliowatarajia Wakusaidie watakugeuzia Mgongo. Usiogope, Usilaumu, Usilalamike Mtumaini Mungu, na Jaribu Njia Nyingine. Mwaka 2016 nilijitoa muhanga wa kutafuta mtaji wa kufanyia biashara. Niliingia kwenye simu yangu nikaona nina namba zisizopungua elfu moja. Katika hizo namba watu Karibu 500 walikuwa wananifahamu. Nikasema ngoja niwatumie watu hawa kukusanya mtaji. Nikaandaa ujumbe mzuri nikawatumia…
478; Farasi Anaweza Kukimbia Sana Ila Sio Peke Yake.
Farasi anaweza Kukimbia umbali mrefu ila hawezi Kukimbia bila mpandaji. Mpandaji ndio atadhibiti mwendo na njia anayotakiwa apite. Bila mpandaji huyu Farasi angeweza kupita kwenye njia zisizo sahihi. Angeweza kuvunjika Miguu kwa Kukimbia kupita kiasi. Mpandaji akiwa mwanafunzi lazima awe na Mwalimu wake. Huwezi kuruhusiwa kwenda porini mbali na Farasi wakati wewe bado ni mwanafunzi.…