Upo hai leo ili ubariki wengine usikubali kua mtu wa makwazo juu ya wengine. Usikubali kua mkosoaji kwa kila kitu mtu anachokifanya bali jaribu kua mshauri tia moyo wengine. Usikubali watu walalamike kua wewe ndio sababu hasa ya kushindwa kwao. Maneno ya kinywa chako yawe baraka yatie moyo wengine yawainue wengine pale wanaposhindwa. Mtu akipitia…
#SiriZaKuaHaiLeo:1. Ni nafasi ya kubadilisha.
Ni nafasi nyingine ya kutubia makosa yako. Ni nafasi nyingine ya kufanya upya kwa umakini pale ulipokosea jana. Ni nafasi nyingine ya kufanya uchaguzi upya. Yako mambo mengi tumechagua jana kwa makosa mengine yana uwezekano wa kuchagua upya leo ndio wakati wake. Ni nafasi nyingine ya kipatana na uliowakosea. Inawezekana jana umekwazana na watu leo…
Walioshindwa.
Walioshindwa jambo na wakaliacha kabisa bila kurudia au kujua kwamba wao wanahusika vipi katika kushindwa kule, wana maelezo ya kutosha kukushawishi na wewe kwa nini utashindwa. Jihadhari sanaa na watu hawa maana wana uwezo mkubwa wa kuondoa hamasa yako juu ya jambo unalotaka kuliendea. Waelewe hivi: Walishindwa kwasababu ya uelewa wao mdogo juu ya jambo…
Kijana una Fursa za kipekee sana. Muda, Nguvu, na Uwezo wa kufikiri.
Habari za leo ndugu msomaji wa makala hizi. Jana nimepokea ujumbe kutoka kwa rafiki yetu ambaye hua anasoma makala hizi kila siku. Akaniomba niandike kuhusu vijana. Kijana tunaweza kusema ni mtu mwenye umri kuannzia miaka 18 hadi 40. Hivyo kama upo hapo lazima uzitumie vyema fursa hizi. Leo tutaangalia Fursa tulizonazo sisi kama vijana na…
Upo hai ili kulitimiza Kusudi.
Kusudi ni nini?Kusudi ni ile sababu hasa ya kitu kuwepo. Bila Kusudi kuwepo kwa kitu hakuna maana. Kitu cha kwanza cha kutambua kwenye maisha yako ni upo duniani kwa Kusudi lipi. Ukiweza kutambua na ukaanza kuliishi Kusudi hilo maisha yako yatakua ya furaha. Mojawapo ya vitu vinavyowafanya watu wasiwe na furaha duniani ni pale wanapotoka…
UNAHITAJI WATU.
Mwandishi mmoja wa vitabu anaejulikana kwa jina la Zig Ziglar Alisema “To get what you want you must help enough people to get what they want” yaani kupata chochote unachotaka unahitaji kuwasaidia watu kupata vile wanavyotaka. Akiwa na maana kwamba kile unachokifanya kiwe kinagusa maisha ya wengine. Kama biashara unayoifanya haigusi maisha ya watu wengine…
Pale unapohisi.
Pale unapojihisi kukata tamaa ndio sehemu hasa ya kuongeza bidii maana ni matokeo yanavyokwenda kuonekana. Pale unapojihisi kuchoka ndio wakati wa kuinuka tena kwani vita ndio imeanza mapambano ndio yamechanganya uchague kurudi nyuma upotee kabisa au upambane hadi mwisho. Pale marafiki zako wanapokucheka na kukwambia umepotea ndio wakati hasa wa kuonyesha unajiamini na unakiamini vyema…
Tabia za watu wenye Mafanikio.
Tabia ni vile vitendo ambavyo tunavifanya mara kwa mara bila kuacha. Tabia ni vitu ambavyo vimejengeka ndani yetu, kama unavyoweza kuamka na kuswaki kila siku asubuhi bila kuchoka wala kukata tamaa. Kuswaki na kunawa uso asubuhi nayo ni Tabia. Sio rahisi uache na wala ujisikie kuchoka. Hii ni kwasababu umerudiarudia hadi ikajijenga kwenye akili yako…