477; Sio Yako Hadi Pale Utakapoitoa Kichwani.

“Kuna kipindi Fulani nilisafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine kikazi. Nilipofikia kwenye familia moja ambayo ilikuwa inanifahamu. Sikuwa nawafahamu sana watu kwenye ile familia Zaidi ya baba mwenye familia ambaye alikuwa mwenyeji wangu. Wakati naendelea kukaa pale nilitokea kuzoeana na binti yake sana hadi nikaanza kuona hisia za upendo. Kiukweli nilikuwa namheshimu sana mzee yule…

476; Unahitaji Watu Zaidi Kuliko Unavyohitaji Pesa.

Mtu Tajiri kuliko wote duniani kwa haraka haraka ukifikiria unaweza kudhani kilichomfanya akawa Tajiri ni pesa zake au akili zake pekee. Ila ukija kutafakari katika upande mwingine unagundua kwamba ukiwa na pesa pekee bila watu utaishia kuzitumia kwa matumizi yako binafsi. Ukiwa na akili nyingi za kugundua vitu halafu huna watu utaishia kugundua tu lakini…

475; Huu ndio Ukosoaji Ninaoupenda.

Mwanzoni simu za smartphone zilipoanza kuja kulikuwa na tatizo kubwa la simu hizo kutokukaa na chaji. Baada ya muda sio mrefu wakaja watu wakaleta Power Bank ambayo inahifadhi chaji. Tatizo linguine likaanza kuonekana kwenye simu hizi ni vioo kupasuka mara kwa mara. Haichukua muda wakaja na Screen Protector. Yaani unanunua simu halafu unakuja tena unanunua…

474; USHAURI: Unapofika Wakati Unaona Maisha Yako Hayana Maana wala Thamani Tena.

Nilikuwa napitia maisha ya mwandishi mashuhuri kutoka Brazil, Paulo Coelho aliendika vitabu vingi kikiwemo cha The Alchemist. Mojawapo ya jambo gumu alilowahi kupitia maishani mwake ni alipokuwa na umri wa ujana yaani miaka ya 18-20 aliwahi kupelekwa hospitali ya vichaa mara tatu na wazazi wake. Wazazi wake waliziona tabia zake na kufikiri ni mtu aliechanganyikiwa…

473; Mawazo Ya Mungu Si Kama Ya Mwanadamu.

Kuna namna ambavyo wanadamu tumekuwa tunajaribu kumtafsiri Mungu katika uelewa wetu kitu ambacho tunasahau ni kwamba uelewa wetu bado ni wa kibinadamu. Hivyo kwa vyovyote bado tunamtafsiri Mungu kwa viwango vyetu. Kama Upumbavu wa Mungu ndio hekima ya mwanadamu basi sisi hatuwezi kusema sana juu yake kwasababu bado tutakuwa tunakosea. Yeye aliumba miti ya matunda…

472; Mbinu za Kuweza Kuwa na Furaha Wakati Wote.

Kuna utafiti ulifanyika wa kidunia ukaja na majibu ya nchi zinazoongoza kwa kukosa furaha duniani. Mojawapo ya nchi iliyotajwa ilikuwa ni nchi ya Tanzania, kwasababu mimi ni mtanzania sikuwa na majibu sahihi wala utafiti wa kupinga hili ila ninaweza kukuandikia wewe mambo machache ambayo unaweza kufanya na yakakuletea furaha binafsi. Watu wengi wamekuwa wanafikiri kwamba,…

471; MAMBO 7 WANAYOFANYA MASKINI LAKINI MATAJIRI HAWAYAFANYI KABISA.

Kinachokufanya uendelee kubaki hapo ulipo ni kwasababu unataka kufanya kile ambacho kila mtu anafanya na atakikubali. Unajua hata ukileta bidhaa yako sokoni ikakubaliwa na kila mtu hiyo bidhaa inashuka thamani haraka. Unatakiwa ukubali kuwa wa pekee hataka kama watu watakuchukia basi iwe hivyo kwasababu wewe sio kila mtu. Kuna neon moja linatajwa sana kwenye maelezo…

470;USHAURI: MUONDOE CHUMA ULETE HUYU KWENYE PESA ZAKO.

Mojawapo ya vitu vinavyowafanya watu waishi maisha ya magumu sana hapa duniani ni kukosa namna bora ya kupangilia na kuendesha maisha yao. Kingine ni kwamba wengi wanapenda kuishi maisha ya kuiga, kwasababu umeona jirani yako ana maisha Fulani hivi na wewe unataka uanze kuishi hivyo. Sio vibaya kutamani vitu vizuri kwenye maisha yako lakini ni…

Jacob Mushi

Afya, Hekima na Utajiri

Skip to content ↓