537; Ingia Ndani Zaidi..

537; Ingia Ndani Zaidi..

Watanzania wengi ni wavivu sana kusoma, kabla hujaamini picha ya kichwa cha habari inayosambazwa jaribu kutafuta habari nzima uisome na uelewe. Vichwa vingi vya habari huandikwa kwa namna ya kuvuta wasomaji na bahati mbaya sana wengi wenu huishia kusoma kichwa tu na kufikia hitimisho. Usiwe mwepesi pia kuamini kila kilichoandikwa kwasababu kwenye ulimwengu wa sasa…

536: Huwezi Kuwaridhisha.

536: Huwezi Kuwaridhisha.

Watu wanaweza kukuchukia pasipo na sababu yoyote ya msingi. Inawezekana hata hujawahi kuwasemesha lakini wakakuchukia. Inawezekana hujawawahi kuwatendea jambo lolote lile baya au la kuudhi lakini wakakuchukia tu. Unapaswa tu kutambua kwamba hata ufanye mambo mema kiasi gani hapa duniani huwezi kupendwa na kila mtu. Huwezi kumridhisha kila mtu. Unaweza kuzungumza sentensi moja ikamsaidia mtu…

528; HEKIMA: Hakuwa Wako.

528; HEKIMA: Hakuwa Wako.

Kama alikuumiza kisha akaondoka hakuwa wako. Au tunaweza kusema muda wake wa kuendelea kuwepo kwako ulifika na njia ya kuondoka kwa ilikuwa lazima wewe uumie kwasababu haukujiandaa kuondoka kwake. Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu. 1 YOHANA.…

527; HEKIMA: Kinyozi Anapokosea Kukunyoa.

527; HEKIMA: Kinyozi Anapokosea Kukunyoa.

Kinyozi anapokosea kukunyoa bila kujali amekosea kiasi gani siku zote baada ya muda Fulani nywele huota tena na utaweza kunyoa vile unavyotaka. Unapopoteza fedha haijalishi ni nyingi kiasi gani kama ni wewe mwenyewe ulizitafuta basi utaweza kuzipata tena. Unapoachwa na mpenzi ambaye ulimpenda sana bila kujali alikuwa mzuri kiasi gani, bado ipo siku utakuja kukutana…

526; HEKIMA: Sumu Niliyowekewa Kwenye Chakula.

526; HEKIMA: Sumu Niliyowekewa Kwenye Chakula.

“Ilikuwa ni siku za mwisho wa mwaka ambapo tulikuwa na utaratibu wa kwenda kuwasalimia ndugu na jamaa ambao hatujawaona miaka mingi. Katika kuwatembelea ndugu jamaa na marafiki wengi siku moja nikapitia kwa ndugu mmoja ambaye hatukuonana muda mrefu sana. Huyu ndugu baada ya kunipokea alinisisitiza sana nile chakula. Nilimkatalia kwasababu nimepita nyumba nyingi na nimeshakula.…

525; HEKIMA: Ni Wewe.

525; HEKIMA: Ni Wewe.

Ni wewe utawajibika pale unapoingia kwenye matatizo bila kujali ni nani aliyeyasababisha. Ni wewe utatakiwa kuchukua hatua pale mambo yanapokuwa magumu kwasababu ya uzembe unaoufanya sasa. Ni wewe utakalipa gharama za ulaji mbovu unaokula sasa pale utakapoanza kusumbuliwa na magonjwa. Ni wewe utakaelipa gharama ya ujinga unaoundekeza sasa hivi, unaambiwa ujifunze hutaki, Unaambiwa uweke akiba…