#SITAISHIA_NJIANI ✈-Napiga hatua kuelekea mafanikio yangu. ❗-Navumilia kila hali na changamoto nitakayopitia njiani. ?-Najifunza kila siku na kuweka kwenye matendo yale ninayojifunza. ??-Naweka juhudi na bidii kwenye kila ninachokifanya kwa mikono yangu. Mafanikio ni Haki Yangu. Eeh Mungu niwezeshe. ?Mimi ……… Unawahitaji watu wote kwenye maisha yako kwasababu kila mtu ana jambo akilifanya kwako lin…
All posts in USIISHIE NJIANI
HATUA YA 248: Unaambatana na Nani?
Ni bora mara elfu kukaa ndani peke yako kuliko kuambatana na marafiki wapumbavu. Ni bora kuishi ndani ya nyumba peke yako kuliko kujichanganya na makundi yasiyofaa. Haijalishi una maono makubwa kiasi gani, au ndoto kubwa kiasi gani unaweza kuharibu mwelekeo wako kwa kupitia aina ya makundi unayoambatana nayo. Kuna watu hawakufai hata kidogo kwenye maisha…
#USIISHIE_NJIANI: KAULI ZA KUJISEMESHA ASUBUHI ILI USIISHIE NJIANI.
Unavyoanza siku yako ndivyo inakwenda kuwa siku nzima. Kama ulianza kwa kugombana na wengine basi ujue siku yako yote itakuwa ni ya kukosana na wengine. Inawezekana umekuwa unasema hii siku imekuwa na mikosi kumbe ni wewe mwenyewe ulianza vibaya siku yako. Inawezekana ukalalamika na kuona siku imekuendea vibaya kumbe ni namna ambavyo ulianza bila ya…
HATUA YA 247: Watu Wanapenda Hali Walizozizoea.
Unajua ni kwanini watu hawapati mabadiliko kwenye maisha yao? Au wakianza jambo Fulani baada ya muda mfupi wataacha na kurejea katika hali ile ya kawaida? Inawezekana na wewe ni mmoja wa watu wa aina hiyo unapaswa kutambua kwamba binadamu wanaogopa mabadiliko. Ndio maana ukitaka kutoka kwenye hali ambayo upo kuna watu wataanza kukupinga na kukukatisha…
#USIISHIE_NJIANI: UTAKULA MATUNDA YA KINYWA CHAKO.
Habari rafiki. Utakula matunda ya kile unachokizungumza kwenye midomo yako. kile unachojinenea kila wakati ndio utakula matunda yake. Hakuna jambo ambalo unazungumza lisitokee tatizo ni kwamba wakati linatokea unakuwa umeshasahau kama ulishajinenea. Nionyeshe mtu mwenye mafanikio anaelalamika, hakuna mtu wa namna hiyo. Kwanza hana huo muda wa kulalamika. Vile unavyojisemea unavyojitamkia ndivyo utakavyokuwa. Anza kubadilisha…
HATUA YA 246: Ukweli Unauma.
Ukitaka watu wakuchukie waambie ukweli. Ukitaka kupingwa na kila mtu simamia ukweli. Ukitaka kupata wafuasi wachache wewe simamia ukweli wale wanaopenda kudanganywa wataona huwafai. Mara nyingi jambo ambalo linapata wafuasi wengi sana kwa haraka huwa najaribu kuangalia kwa macho ya ziada kama ni la kweli kwasababu wengi wengi hatupendi ukweli. Mara zote tunapenda mambo marahisi…