Unapokuwa mtu wa mawazo hasi unaweza kupita mahali ukawakuta watu wanacheka halafu ukaanza kuhisi kwamba wanakucheka wewe. Pia unaweza kuwakuta mahali watu wanazungumza kisha walipokuona wakanyamaza wewe kwasababu huwa unafikiri hasi tu kila saa unaanza kuhisi hawa watu walikuwa wananisema mbona wamenyamaza waliponiona? Mtu mwenye fikra hasi anaishi Maisha ya tabu sana, anateseka kila wakati.…
All posts in MAFANIKIO MAKUBWA
SURA YA 431; Tai Alievunjwa Mbawa.
Siku Moja Mzee aliekuwa anafuga kuku kwenye Kijiji fulani, alikuwa anapita porini akaokota yai kubwa ambalo hakuelewa ni la Ndege gani. Aliamua kulichukua yai lile na kuliweka katika mayai yaliyoanza kuatamiwa siku za Karibuni. Baada ya siku kadhaa kupita yule kuku akawa anatotoa mayai yake na kama muujiza hivi na lile yai kubwa likatotolewa. Kumbe…
SURA YA 430; Huwezi Kumkwepa Mtu Huyu.
Unaweza kumdanganya kila mtu kadiri ya uwezo wako lakini yupo mtu mmoja ambaye siku zote atakuwa anakutazama na kusikitika kwa kile unachokifanya na mtu huyu ni wewe. Unaweza kujaribu kukwepa watu ambao umewafanyia ubaya, ukawakimbia wanaokudai, ukawakimbia wanaokusema vibaya lakini wewe binafsi huwezi kujikwepa. Hivyo basi mtu ambaye unapaswa kuhakikisha anakuwa mtu mwema, anaewapenda wengine,…
SURA YA 429; Unaongozwa na Akili Yako, Ikidhoofu Itakuongoza Wapi?
Matendo yetu yote yanaongozwa na akili kama akili zetu zitakuwa hazina afya basi tutakuwa tunapata matokeo mabovu kila wakati. Unaweza kuendelea kulalamika kuwa hupati matokeo unayoyataka lakini nakusihi uanze kutazama akili yako huwa unaijaza vitu vya aina gani. Kile kilichojaa sana kwenye akili yako ndio kinakuwa sababu ya matokeo unayopata. Mwaka huu punguza kabisa vitu…
SURA YA 428; Ukitegemea Hiki Pekee Utachoka Haraka.
Mwanadamu pekee aliekuwa na akili sana kuliko wanadamu wengine ni Adamu na yeye alipewa uwezo huo kwasababu alikuwa peke yake. Hivyo kwa akili na uwezo aliokuwa nao ukamuwezesha kuyaendesha Maisha yake kwa urahisi. Kwasasa kila unachotaka kukifanya kwa kiasi kikubwa kinategemea wengine, inawezekana ni vifaa, au hata watu wengine utawahitaji ili uweze kuwa na ufanisi…
SURA YA 427; Njia Rahisi ya Kuwavuta Watu Sahihi Kwako.
Tupo kwenye dunia ambayo ni ngumu sana kumjua mtu kwasababu wengi wamevaa mavazi yanayofunika uhalisia wao. Wamevaa tabia za kuigiza ambazo sio za kweli na wala hawana kabisa. Wamevaa Maisha ambayo ni uongo na ndani yake wanateseka huku wakifurahia kuona watu wanawasifia. Sasa ili uweze kuwavuta watu sahihi na kuwaacha hawa waliojivalisha mavazi ya uongo…