407; Naomba Nikukumbushe tena Hili.

Yapo mambo ambayo ni msingi wa Maisha bora ya kila mwanadamu, kama ukiweza kuyafanyia kazi vizuri utaishi kwa furaha na amani hapa duniani siku zote. Ni kweli yapo mambo mengi mabaya yanatokea bila sisi kujua na tunakuwa hatuna uwezo wa kuzuia lakini ukiweza kufuata hii misingi utaweza kuwa na Maisha bora. Mambo haya ndio yanayofanya…

406; Ni rahisi Sana Kuanza, Tabu Ipo Hapa.

Watu wamekuwa wanasema mwanzo ni mgumu ni kweli kuna baadhi ya mambo mwanzo ni mgumu. Ila bado kuna mambo ambayo ni rahisi sana kuanza ila kumaliza vile ambavyo unataka ndio imekuwa changamoto ya wengi. Unaweza kuwa na mawazo makubwa na mipango mikubwa wakati unaanza mwaka lakini unapofika mwisho unajikuta hujafanya hata robo ya kile ambacho…

405; Sio Lazima Ufanane Nao

Furaha itakuja pale ambapo utaanza kuishi Maisha ambayo moyo wako unataka na sio vile ambavyo watu wanataka uishi. Furaha ya kweli ipo ndani yako na utaweza kuipata kwa kuishi kile ambacho Mungu ameweka ndani yako. Hakuna haja ya kuishi Maisha vile ambavyo jamii inakulazimisha wewe uishi, vile jamii ambavyo imetengeneza na kutoa maana ya Maisha.…

404; Ni Wachache Sana Wanaweza Kujibu Swali Hili.

Ukimuuliza mtu akutajie mambo 3 ya muhimu sana kwenye Maisha yake ni wachache wataweza kukujibu kwa usahihi nikiwa na maana kwamba walikuwa wanayajua kabla hujawauliza. Ni rahisi mtu kujibu kwa kutamka kile ambacho kitamjia kichwani kwa wakati huo lakini ukweli ni kwamba utakuta hafanyi chochote katika hayo aliyosema ni ya muhimu kwenye Maisha yake. Embu…

403; Maneno Yao Sio Uhalisia Wako.

Wanaweza Kusema yule jamaa alifeli shule hajaweza kufika hata chuo hawezi chochote. Wanaweza kusema yule dada kila mahusiano yamemshinda hawezi kutulia na mwanaume. Wanaweza kusema pia pombe zitakuja kukuua siku moja. Wanaweza kusema wewe ni mtu wa maneno maneno sana na huwa unaongea vitu visivyoeleweka. Hayo yote na mengine ambayo wanaweza kusema juu yako ni…

402; Mtu Huyu Anakudanganya.

Ulishawahi kutaka kukutana na mtu akakujibu kwamba hana muda? Umewahi kujiuliza ni kwanini anasema hana muda? Je kuna ukweli wowote pale anapokwambia hana muda? Wanadamu wote tumepewa masaa 24 kila siku na hii ni mojawapo ya vitu ambavyo kila mmoja anacho kwa usawa kabisa. Kinachotutofautisha ni yale ambayo tunatumia kwenye muda wetu kila siku. Kuna…