SURA YA 426; Hii Ndio Sababu Ya Wewe Kuanza Vizuri na Kumaliza Vibaya.

Hongera sana kwa kuona mwaka mpya, nafurahi pia kuona umesoma Makala hii kwa mara ya kwanza kwa mwaka 2019. Nimekuwa nahudhuria mikesha na matamasha ya kuingia mwaka mpya na siku zote nimekuwa najifunza kitu ambacho kimekuwa kinajirudia sana. Hakuna mwaka ambao umewahi kutabiriwa mabaya, na hata kama watasema utakuwa mwaka wenye magumu lazima watayataja mazuri…

TUSEMEZANE 424; Ukimpata Usikubali Aondoke.

Katika Maisha tunakutana na watu wa aina mbalimbali wanaweza kuwa wabaya kwetu na wengine huwa baraka kubwa sana kwenye Maisha yetu. Unaweza kukutana na mtu wa pekee sana kwenye Maisha yako na usiweze kujua kwasababu shetani amefunga ufahamu wako usione huyu mtu ni wa namna gani. Ni vyema ukawa na uwezo wa kufahamu wale watu…

NGUVU MPYA 423; Usikae Hapo Muda Mrefu Sana.

Unaweza kufanya mambo makubwa kwenye Maisha yako na ukashindwa kusogea mbele tena kwasababu moja ya kulewa na yale matokeo. Jambo ambalo tayari umeshalifanya na ukashinda halitakiwi liwe ndio jambo unaloliongelea sana kwamba umelifanya. Waachie wengine walizungumzie wewe nenda katafute jambo jingine kubwa Zaidi la kufanya. Sijasema usifurahie matokeo uliyopata bali nasema usifurahie sana hadi ukasahau…

NGUVU MPYA 422; Eneza Habari Njema.

Watu wamekuwa ni mashujaa sana wa kueneza habari mbaya kuhusu wengine, imekuwa ni desturi yetu pia kutoa vipaumbele Zaidi kwenye habari mbaya kuliko njema. Wafuatiliaji wa habari na watoaji wa habari wote wamekuwa wakipendelea Zaidi habari mbaya. Kwenye Maisha yako kama unataka kufanya jambo lenye kuacha alama basi chagua kusema kile ambacho kinawasaidia wengine. Habari…

NGUVU MPYA 421; Aibu Ya Makosa Uliyokwisha Kuyafanya…

Katika Maisha mwanadamu anapitia mambo mbalimbali sana, kuna mengi mtu unakuwa umeyafanya mengine ni ya aibu sana. Kikawaida mambo haya yanaweza kuwa kikwazo kikubwa kwa wewe kusonga mbele kwasababu yanakuwa kama yanakurudisha nyuma. Unaogopa watu watajua wewe ulishatoa mimba ndio maana unashindwa kufanya mambo makubwa. Unaogopa watu watajua kuwa ulibakwa ulipokuwa mdogo na ndio maana…

NGUVU MPYA 420; Unahitaji Vitu Hivi 3 Uwe na Maisha Yenye Furaha.

Maisha yanajengwa kwa misingi, Maisha mabovu yamejengwa kwenye msingi mbovu, Maisha bora yamejengwa kwenye msingi imara na bora. Ifahamu misingi ya Maisha unayoyataka na kisha uanze kuifanyia kazi kila siku. Kuna matatizo yanaweza kuwa yanakuandama kwenye Maisha kwasababu tu hujaifahamu misingi na kanuni za Maisha. Na suluhisho ni kuzifahamu kanuni na misingi kisha uanze kuzifanyia…

Subscribe