HATUA YA 261: Ni Kweli Huna Muda?

Ukiona mtu anakwambia hana muda au yuko bize sana wala usiumize kichwa sana unatakiwa ujue kwamba huyo mtu hajaamua kulipa lile jambo lako kipaumbele au hajaamua kukupa wewe kipaumbele. Inawezekana mtu ana majukumu mengi sana ya maisha yake kiasi kwamba anashindwa kufanya mambo mengine ambayo anapaswa kuyafanya kweli lakini pale linapokuja swala la msingi katika…

HEKIMA YA JIONI -2

Ukisema unangoja mambo yawe mazuri ndio ufanye biashara, au ununue kitabu, au uanze kile kitu ulichokuwa unakitaka nikwambie ukweli unajidanganya. Kama hiyo hali mbaya uliyonayo sasa hivi haijaweza kukufanya ufanye maamuzi ya kuanza kile unachokitaka usitegemee hali ikiwa nzuri ndio utachukua hatua. Zaidi sana hali ikiwa nzuri ndio utasahau kabisa hata kama kuna watu huwa…

HEKIMA YA JIONI-1

Watu wengi wamekuwa waoga hasa pale wanapojilinganisha na wengine na kujiona wao ni wa kawaida na hivyo kushindwa kujitambulisha vyema wanapokutana na wengine. Unaweza kufanya makossa ukapoteza wateja wapya ambao ungewapata kwa kusema tu unachokifanya, hata kama huna ofisi usiogope kusema unafanya biashara gani. Kuwa Mfuasi wa Kwanza wa Ndoto zako, usisubiri hadi watu waanze…

HATUA YA 260:  Vitu Hivi Unavyoviruka Vitakutesa Baadae.

Kuna michezo kama hukuicheza ukiwa mdogo huku ukubwani itakuja kukusumbua. Hili lina ukweli wake kiasi Fulani japo sio kwa mambo yote. Tukija kwenye upande wetu wa maisha kuna mambo ambayo unaweza kukutana nayo na ukayaona ni magumu bora uachane nayo. Ukweli ni kwamba huko baadae yatakuja kukusumbua. Kuna sehemu utashindwa kuzifikia kwasababu ya hatua ulizoziruka.…

HATUA YA 259: Ni Dharau au Ni Hisia Zako.

Nimezoea kuona watu wengi ambao wako chini kwenye vitu Fulani kuwaona wenzao waliowapita kama wana dharau sana. Mfano mtu mwenye bodaboda atasema watu wenye magari wana dharau na hawawajali bodaboda. Vilevile maskini ataona matajiri wengi wana dharau, wanajisikia, wanajiona, hawawapendi maskini. Ni wachoyo na mengine mengi. Kama na wewe umeshakuwa na hisia kama hiyo kuona…

HATUA YA 258: Moyo Wako Uko Wapi?

Mojawapo ya sababu ambazo zinawafanya watu waharibu kazi za wengine ni kufanya kazi huku mioyo yao iko sehemu nyingine kabisa. Wewe umekuwa mwalimu kwasababu uliona ndio utapata kazi kirahisi lakini moyo wako uko kwenye kilimo siku zote utakuwa ni mwiba kwa wanafunzi. Biashara nyingi zimekosa maendeleo n ahata mafanikio kwasababu ya hawa watu ambao wanafanya…