Your Positive Action Combined with Positive Thinking Results in Success. – Shiv Khera Matendo yako chanya yakijumuishwa na mawazo yako chanya yanaleta matokeo kwenye mafanikio. Kama unataka kufanikiwa lazima uzitangatie mambo haya mawili, mawazo chanya na matendo chanya. Kama utakuwa na mawazo chanya peke yake bila ya matendo huwezi kupata matokeo mazuri ya mafanikio. Vilevile…
All posts in HATUA ZA MAFANIKIO
HATUA YA 290: Heri Ya Mwaka Mpya
Habari Rafiki yangu mfuatiliaji wa Makala hizi za HATUA. Kila mmoja anayofuraha na jambo la kusema asante kwa Mungu alietupa uzima na tumeweza tena kuona mwaka huu 2018. Pamoja na mengi sana ambayo ulipitia mwaka jana magumu kwa namna yeyote ile tafuta mema ambayo unaweza kusema ni shukrani kwa Mungu. Kwanza kuwepo hai pekee ni…
HATUA YA 289: Shughulika na Hiki 2018
Mara nyingi tumekuwa tunapambana na mambo ambayo hayaondoi matatizo yetu bali yanayapooza tu na kisha baada ya muda hujirudia. Kama kuna sehemu inavuja kwenye nyumba yako suluhisho sio kukinga maji yanayodondoka bali ni kuziba pale panapodondosha maji. Watu wengi tumekuwa tunatatua matatizo yetu kwa mfumo huu wa kutega ndoo kukinga maji yanayovuja badala ya kuziba…
HATUA YA 288: Upo Tayari?
Unachokifanya sasa hivi kama kinatoka ndani ya moyo wako upo tayari kukifanya hadi unakufa hata kama hutapata chochote? Hili limekuwa ni swali moja gumu sana kujua kama watu wanaosema wanapenda wanachokifanya wanapenda kweli au ni maneno. Kama utakosa chochote kusifiwa, kulipwa, kupongezwa na bado ukaendelea kufanya inaonyesha kweli umejitoa kufanya kile unachokifanya. Je upo tayari…
HATUA YA 287: Unachokisema na Unachokifanya.
Siku zote ili upate kile unachokitaka inatakiwa unachokisema kiendane na unachokifanya. Na kama ukiona maneno yako ni tofauti na unayoyafanya kila siku ujue umeshapotea. Kama unapenda mafnikio anza kufanya vitu vitakavyokupeleka kwenye mafanikio. Kama unataka pesa acha kufanya starehe achana na msemo usemao tumia pesa upate pesa badala yake anza kutumia pesa kwenye vitu…
HATUA YA 286: Mwogope Mhitimu Huyu Popote Utakapokutana Nae.
Mojawapo ya sifa kubwa ambayo inamtofautisha mwanadamu na viumbe wengine ni kufikiri. Na sio kufikiri tu na baada ya kufikiri kufanya maamuzi ambayo yatamwezesha aendelee kuishi. Ili uweze kufikiri sawasawa ni muhimu sana kama binadamu uwe na tabia ya kuweza kujifunza ili usiwe kama viumbe wengine ambao uwezo wao wa kufikiri siku zote unafanana. Mtu…