Ukweli ni kwamba ukitafuta kueleweka utakuwa unawachanganya watu badala ya watu kukuelewa. Kitu ambacho unaweza kukifanya pekee ni kuendelea kufanya kile unachoamini, endelea kuwa wewe hata kama watu wanakupinga. Kutaka kueleweka na kila mtu ni kazi ngumu sana ambayo wengi walishashindwa. Ukianza kuishi kile unachokiamini kuna watu wengi wataendelea kukufuata kwasababu wataanza kuamini kile unachokifanya.…
HATUA YA 384: Unahitaji Kuwa na Watu Hawa Wa Muhimu.
Mafanikio yako yamebebwa na watu wengine. Ili uweze kufika mbali lazima uwajue watu ambao ni sahihi kwenye mafanikio yako. Pesa unazozihitaji zipo kwa watu sasa ni jukumu lako kujua ni watu hasa wanazo pesa zako. Na sio kuishia kujua tu ni lazima kwanza uwe umejua wewe una kitu gani ndani yako ambacho kitakuongoza kuwajua watu…
HATUA YA 383: Ni Haki Yako Lakini Lazima Uumie
Unajua kila kitu kizuri hapa duniani ni kwa ajili ya kila binadamu? Unajua kwamba hata wewe unastahili dhahabu, ndege, au chochote kizuri? Unajua kila ambacho umekuwa unakitamani kwenye akili yako ni sawa kabisa? Ni kweli ni haki yako, mafanikio ni haki yako, utajiri ni haki yako, kuwa mtu mkuu ni haki yako. Lakini sasa ili…
HATUA YA 382: Njia Pekee ya Kuiponya Dunia Hii.
Pamoja na matukio maovu ambayo yanaendelea kila siku hapa duniani, tunasikia watu wanauwawa kinyama, wengine wanafanyiwa Matendo mabaya sana kama ubakaji, na mengine unayoyafahamu ipo njia moja ambayo kila mmoja akiweza kuifanya anaweza kuiponya dunia. Pamoja na kuwa mambo haya yanaumiza sana kiasi kwamba unaweza kuwaza kufanya mambo mabaya sana lakini hiyo haitasaidia maana ukifanya…
HATUA YA 381: Wewe Unaona nini Kwenye Vitu/Watu?
As Confucius said: Everything has its beauty, but not everyone sees it. Confucius alikuwa ni mwanafalsafa wa Kichina aliwahi kusema kwamba kila kitu kina uzuri wake lakini sio kila mtu anaweza kuona uzuri kwenye kila kitu. Na huu ndio ukweli hata kama mtu ni mbaya kwa kiasi gani bado kuna sehemu atakuwa mtu mzuri. Unaweza…
HATUA YA 380: Fuatilia Maisha ya Watu Hawa..
Usipoteze muda wako hata kidogo kufuatilia Maisha ya mtu ambaye wewe binafsi huna mpango wa kufika pale alipo. Itakuwa ni sawa na mtu anaetaka kupungua lakini hajui ni vyakula gani hasa anatakiwa ale ili asiendelee kuongezeka unene. Lazima ujue ni vitu gani ulishe ubongo wako, na huwezi kujua vizuri kama huna mahali unataka kufika. Tafuta…
HATUA YA 379: Ni Kipi cha Muhimu Kwenye Maisha Yako?
Kipaumbele kikubwa kwenye Maisha yako ni kipi? Ndugu yangu kama huna kipaumbele kikuu cha Maisha ambacho ndio kinakuwa sababu ya wewe kuamka mapema, kufanya kazi kwa bidii utakuwa unapoteza muda. Lazima Rafiki uwe una kitu cha muhimu la sivyo Maisha yako yatakuwa ni dharura tu. Usiishi Maisha ya kufanyia kazi vitu vya dharura vinavyotokea kwenye…
HATUA YA 378: Kama Ukiamka Asubuhi Unafanya Kitu Hiki, Upo Kwenye Hatari Kubwa Sana.
Muda wa asubuhi ndio wakati ambapo akili yako inakuwa na uwezo Mkubwa sana wa kufikiri na kufanya maamuzi magumu. Kama ukiweza kuutumia muda huu vizuri kufanya yale ya muhimu kwenye Maisha yako utakuwa na maendeleo makubwa sana. Watu wengi wanapoamka asubuhi kitu cha kwanza kufanya ni kushika simu zao kuangalia ni nani amewapigia au kuwatumia…