#HEKIMA YA LEO : Ushindi Mdogo ni Ushindi Mkubwa.

Habari Rafiki, Leo ni siku nyingine tena ambayo tumepewa kama zawadi kwa ajili ya kwenda kuyafanya Maisha yetu yawe bora Zaidi.

Jisemeshe Maneno Haya Kabla Hujatoka Kwenda kufanya Chochote.

“NACHUKUA HATUA, NAJIFUNZA, NAWEKA JUHUDI NA BIDII, NAVUMILIA.

MAFANIKIO NI HAKI YANGU, EEH MUNGU NIWEZESHE.”

Usidharau Kile kidogo unachokifanya. Daudi alijua kwamba anaweza kumpiga Goliath baada ya kutazama kule alipokuwa. Kujaribu kwake kupambana na dubu kulimpa nguvu kwamba hata Goliath si kitu mbele yake.

Ushindi mdogo mdogo unaopata kila siku ndio unakuonesha kuwa unaweza kufanya makubwa zaidi.

Ni ngumu kuamini unaweza linapokuja jambo kubwa, kama hujawahi kufanya jambo dogo ukapata ushindi.

Hapo hapo ulipo sasa hivi kuna vitu unaweza kuvifanya weka nguvu zako zote. Weka uwezo wako wote. Ipo siku utatumia hivyo vitu kama njia ya kupata makubwa zaidi

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.co.tz/vitabu/

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.co.tz/huduma/

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.co.tz/jarida/

Get new articles

I’ll send you new articles as soon as they come out — by email, WhatsApp, or both.

Fill in either one, or both.

Toa maoni yako

Barua pepe yako haitaonyeshwa.

Chukua hatua moja leo.

Kila kitabu nilichoandika kimezaliwa kutoka makala kama hii. Kama kuna unachotaka kunieleza, niandikie.

Jiunge Nunua Kitabu