Biashara

Sikuanza na mtaji. Nilianza na wazo, laptop na chumba kimoja Mbagala. Hizi ndizo kampuni na chapa zilizotokana na wazo lile.

  • Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji · 2018

    NETPOA LIMITED

    Hosting, usajili wa domain na huduma za kidijitali kwa biashara na taasisi za Tanzania. Ilianzia chumba kimoja Mbagala. Leo ni miongoni mwa kampuni bora za hosting nchini, ikihudumia zaidi ya wateja 1,000 — tovuti, barua pepe za kampuni, SSL na domain za .co.tz.

Nikiwa chumbani kwangu Mbagala, nikiwa na laptop na godoro pekee, nilibuni jina “Netpoa”. Hakuna aliyekuwa amelitumia.

Unataka kujenga kitu chako?

Kuanzia jina la biashara hadi kurasimisha kisheria na kuwa mtandaoni — niandikie, nikuelekeze hatua zinazofuata.