Moja ya jukumu kubwa nililojipa kwa mwaka huu 2017 ilikuwa ni kujifunza kwenye Maisha yaw engine, na hapa ni kuona namna gani wanavyoendesha Maisha yao kuanzia ndani hadi nje. Yapo mengi sana kama binadamu unaweza kujifunza kwenye Maisha ya wenzako kwasababu tumeumbwa tofauti, tumekulia kwenye mazingira tofauti na kila mmoja ana kusudi la yeye kuwepo…
All posts in USIISHIE NJIANI
USIRUDIE TENA AU USIJARIBU KOSA HILI MWAKA 2018
Katika Maisha tunakutana na watu ambao wanaweza kuwa baraka sana kwenye Maisha yetu hadi tukajisahau kwamba kuna siku wataondoka. Ninaposema kuondoka simaanishi kufa namaanisha kuna siku hawatakuwa pamoja nasi kama walivyokuwa nasi mwanzo. Kosa ambalo unaweza kulifanya na likasababisha uje kujuta Maisha yako yote ni kuwapa utegemezi mkubwa watu ambao hawadumu maishani mwako. Lazima ujifunze…
HATUA YA 269: Huhitaji Kikubwa Sana.
Mara nyingi tunafikiri ili ufikie hatua kubwa kwenye maisha lazima uanze na mwanzo ambao ni mkubwa sana. Usifikiri kwamba ukiwa na vitu Fulani na Fulani basi ndio maisha yako yatakwenda vizuri. Kama umeshindwa kutumia rasilimali ulizonazo sasa hivi hata ukipewa kubwa bado utashindwa na unaweza ukaharibu badala ya kutengeneza. Uwezo wako unapimwa kwa namna ambavyo…
HATUA YA 268: Swali La Kujiuliza Unapojua Unachokitaka.
Kujua kile unachokitaka ni jambo la kwanza, kinachofuata ni kufahamu gharama ambazo unapaswa kulipa ili kufika pale unapotaka. Wengi wanaishia kwenye kujua wanachotaka na kukata tamaa baada ya kuambiwa gharama wanazotakiwa kulipa. Ni vyema ukajiuliza maswali haya na ukapata majibu yake wakati unaanza safari yako. Unajua gharama gani unapaswa kulipa ili ufike unakotaka kwenda?…
HATUA YA 267: Nipo Hapa tangu 96!
Siku moja nikiwa maeneo ya stand nikakutana na watu wawili wakigombania Tsh elfu mbili mmoja katika hasira sana akamwambia mwenzake wewe mbona unakuwa kama umekuja stand jana? Kwa hasira sana mwenzake akajibu kwamba nipo hapa tangu mwaka 96 nikashangaa sana kuona watu sh elfu mbili inawafanya wajivunie kuwepo kwenye kitu kile kile bila ya mabadiliko…
HATUA YA 266: Hili Ndio Bomu Unalojitengenezea Kila Siku.
Katika Maisha vipo vitu vingi tunafanya mara nyingi ni kwa kuiga yale ambayo wengine wanafanya, mengine tunaangalia tangu zamani walikuwa wanafanya na mengine ni asili yetu yaani unafanya kwasababu ndio asili ya kila kiumbe hai. Shida inakuja kuwa kubwa sana pale unapokuwa unafanya jambo kwasababu watu wengine wanafanya. Hapa ndipo unakuwa unajitengenezea bomu kubwa sana…