Usiwe na Tabia za Maji.

Maji hayana umbo wala rangi, ukiyaweka kwenye chombo chochote kile yatachukua rangi ya chombo na umbo la chombo. Ukiyamwaga chini yatachukua vilevile rangi ya pale uliyoyamwaga. Maji siku zote hayana utaratibu yanafuata mkondo uliopo mbele na kuanza kutiririka. Pia yasipowekewa utaratibu mzuri huleta uharibifu mkubwa. Maji hayawezi kupanda mlima siku zote yanakimbilia mabondeni, ukitaka kuyapandisha…

Unajisogeza Kwenye Shimo…

Mafanikio hayamtaki mtu mvivu, mtu mzembe, anaeahirisha mambo, anaetazama Zaidi kule alipotoka kuliko anapokwenda. Mafanikio yanamtaka mtu ambaye ameamua kutoka moyoni mwake kuwa anayataka mafanikio. Usikubali kabisa kuingia kwenye mtego wa kuchanganya mambo, kama umeamua kuwa muumini wa mafanikio amua kweli na uzifuate kanuni na misingi. Ukiwa mtu wa kuchanganya mambo, leo unataka hiki kesho…

JINSI YA KUISHINDA TABIA YA KUISHIA NJIANI KWENYE MAISHA YAKO.

Tabia ya kufanya jambo kidogo kisha ukaona hakuna matokeo na ukakata tamaa na kwenda kukimbilia kufanya jambo jingine inaweza kuwa sababu ya wewe kutokutimiza chochote kwenye Maisha yako. Kama huna uwezo wa kufanya jambo moja hadi ukahakikisha limekuletea matokeo anza mapema kuitengeneza. Zipo sababu nyingi unaweza kuwa nazo za kwanini umeishia njiani lakini ukweli sababu…

Jinsi Ambavyo Kuchelewa Kufanya Maamuzi Kunavyoweza Kukuongezea Ugumu Wa Kufanya Maamuzi.

Katika mambo ambayo yanaweza kuwa sababu ya kila mtu mwenye mafanikio kufika pale alipo ni tabia hii ya kufanya maamuzi kwa wakati. Kama umeambiwa tafiti zinasema mwaka huu mvua hazitanyesha nyingi hivyo watu wapande mazao yanayovumilia mvua. Halafu wewe ukakazana kubaki unasubiria mvua ndugu yangu utakosa vyote au ukija kufanya maamuzi utakosa kiwango ulichopaswa kuvuna…

UnaPata Muda wa Kukaa na Kuongea na Wewe?

“Vile nilivyojieleza kwako kuhusu mimi mara nyingi inaweza kuwa ni vile nilivyotaka wewe unifahamu mimi lakini inaweza kuwa mimi halisi sio huyo niliekuelezea.” Jacob Mushi Tumekuwa tunapata muda wa kukaa na watu, muda wa kazi, muda wa kuperuzi na kujua yanayoendelea duniani lakini mara chache sana tumekuwa tunapata muda wa kukaa na sisi. Kiwango unachojifahamu…