Vile unavyojiona ndani yako ndio kunafanya uwe mtu unaejiamini au mwoga. Kunafanya pia uwe mtu unaethubutu kuchukua Hatua au uwe mtu wa kusitasita na kuahirisha. Namna unavyojiona ndani yako kunaweza kuathiriwa na namna ulivyokuwa tangu ukiwa mdogo. Yale maneno ambayo ulikuwa unaambiwa mara kwa mara yanaweza kuwa sababu ya jinsi unavyojiona sasa. Vilevile unaweza kujiona…
All posts in USIISHIE NJIANI
#HEKIMA YA JIONI; Dunia Haijawahi Kuwa Sawa na Haitaweza Kuwa Sawa.
Kwenye dunia hii haijawahi kutokea hata siku moja kukiwa na idadi kubwa ya watu na watu wote wakawa wanafurahi tu bila matatizo ya aina yeyote. Kuna mambo mengine yanatokea ni mabaya ndio lakini ni kwasababu ya mazuri ambayo yanapaswa kutokea mahali Fulani. Wewe unapovuna mazao mengi shambani na ukapeleka sokoni ukiwa na matumaini ya kupata…
Hiki ndio Kinachotokea Unapokuwa Mtu wa Kutoa Sababu.
Pamoja na sababu nyingi ambazo zinasababisha wewe kuendelea kubaki hapo ulipo, unapofikiri kwamba wewe huna ndugu wa kukusaidia, huna mtaji wa kutosha kuanza biashara, mazingira uliyopo ni magumu, na sababu nyingine nyingi unazojitetea unakuwa unaziba akili yako. Pale tu unapoambiwa kwanini huna fedha za kutosha ukaanza kuwa na sababu kede kede unaifanya akili yako iwe…
Kaa Mbali na Mtu Huyu na Usikubali Kuwa Kama Yeye.
Kwenye Maisha tunakutana na watu wa aina mbalimbali ambao wengine wanaweza kuwa ni marafiki na wengine wanakuwa maadui. Mojawapo ya watu ambao utakutana nao ni watu wanaopenda kupokea bila ya kutoa chochote. Yaani mtu wa aina hii tunaweza kumwita kupe. Mtu wa aina hii anapokutana na wewe ukamwona amehamasika sana anaongea maneno mengi sana ya…
Hali Itakapokuwa Mbaya..
“Kinachokupa Matumaini na Kiburi ni hali nzuri uliyonayo sasa hivi” Bahati mbaya sana unajisahau kwamba unachokitegemea ipo siku kinaweza kuwa na ukomo. Usisubiri hali iwe mbaya ndipo uanze kutafuta njia nyingine ya kipato, Usisubiri Mambo Yaharibike ndipo ukumbuke kuchukua hatua, jiandae mapema kwasababu hakuna anaepanga mabaya lakini siku zote tunayaona yakitukuta. Hali itakapokuwa mbaya ndipo…
Haijalishi Una kipaji Kizuri Kiasi gani Unahitaji Kitu Hiki.
Watu wenye mafanikio makubwa duniani, ambao tunawaona ni matajiri waliweza kugundua siri hii kubwa na ya muhimu kwa kila mtu mwenye wazo au kipaji kizuri ndani yake. Kitakachokufanya ufanikiwe sio uzuri wa kipaji chako, sio sauti yako nzuri ya kuimba, sio watu wengi wanaokujua. Lazima ugundue siri hii ya muhimu, ambayo ndio iliwatoa wengi sana…