Kwa vyovyote vile hata kama utaogopa kufanya mambo yaliyo makubwa, hata kama utaogopa kupoteza pesa zako bado huwezi kuondoka duniani ukiwa hai. Kama unaogopa kupata msongo wa mawazo kwasababu biashara itakusumbua Rafiki yangu hata usipoupata huo msongo wa mawazo bado hapa duniani utaondoka ukiwa umekufa. Hatujui ni kitu gani kitakuondoa duniani hivyo basi wewe endelea…
All posts in MAISHA NA MAHUSIANO
Kufanikiwa au Kufa-2/11/2018
Kama unafikiri kutafuta pesa ni ngumu basi jaribu kukaa bila pesa uone ilivyo rahisi. Naomba nikwambie Rafiki mafanikio sio lelemama yaani sio kitu ambacho kinakuja chenyewe tu lazima uweke juhudi za kutosha. Lazima uwe na nidhamu ya kutosha. Wewe usifikiri ni kama vile ambavyo umeshajizoesha. Kuna vitu vya ziada ambavyo unatakiwa kuvifanya na hujazoea kuvifanya…
Kufanikiwa Au Kufa 1/11/2018
Ukitaka vitu vya tofauti ni lazima ukubali kufanya vitu ambavyo hujawahi kufanya. Kama unataka kufanya vitu ambavyo hujawahi kufanya lazima ukubali kufanya maamuzi magumu ambayo hata watu wa karibu wanaokutazama wanaweza kuogopa. Kama utaendelea kubaki hivyo ulivyo na ukafanya unayoendelea kufanya kila siku maana yake utapata matokeo yale yale na hutasogea mbele hata kidogo. Wanajeshi…
26/10/2018 Maisha Yako Ya Sasa Ni Matokeo ya Kitu Hiki..
Aliwahi kusema Charlie Jones kwamba utakuwa mtu yule yule miaka mitano ijayo isipokuwa watu utakaokutana nao na vitabu utakavyosoma. Hii ina maana kwamba kama utaendelea kubaki na vitu vile vile ambavyo umekuwa unavifanya utaendelea kubaki vile vile. Hii pia ina maana kwamba maisha yako ya sasa ni mchango wa watu ambao umekutana nao miaka 5…
25/10/2018 Uepuke Mtego Huu Uliowaangusha Wengi.
Unapokuwa huna chochote cha thamani huwezi kuona mtu yeyote akionesha kuvutiwa na wewe. Wakati mwingine unaweza kuwa unafanya mambo ya maana sana lakini ukashangaa hakuna mtu anahangaika na wewe. Hakuna mtu atahangaika na wewe kama ulichokibeba hakina thamani. Hakuna mtu atapoteza muda wake kwako kama wewe huna cha maana ulichobeba. Unapoanza kuona unapata marafiki wapya,…
399: Woga Haukusaidii Chochote Hapa..
Umekutana na mtu ukatamani sana kuzungumza nae lakini ghafla yakaanza kuja mawazo kichwani kwako kwamba, “huyu atakuwa anaringa” “mimi sistahili” “nitaongea nae siku nyingine”. Mwishoe unaondoka huku ukiwa hujaweza kuzungumza neno lolote. Huu ni woga na hofu ambayo umejitengenezea mwenyewe. Kwanza unatakiwa ujue hata kama hayo unayowaza ni ya kweli basi yeye ndie ana matatizo…