Kama ulikua hujui kwenye hii dunia kila binadamu anauza. Kila mtu kuna kitu anauza au kama hauzi basi hajajua kama anauza. Unatakiwa ujue ni kitu gani hasa unakiuza ili uweze kukiuza vizuri. Unatakiwa ujue unaemuuzia ni mtu wa namna gani! Hata kama una bidhaa nzuri kiasi gani kama humjui mteja wako huwezi kuuza vizuri au…
All posts in HATUA ZA MAFANIKIO
HATUA YA 24: Kwanini Ulizaliwa Mwanadamu?
Leo nataka ujiulize kwanini Mungu alikuumba wewe mwanadamu na wala sio kiumbe kingine chochote? Ukijua hivyo huwezi kujidharau! Ukijua hivyo huwezi kujifananisha na wengine! Ukijua hivyo huwezi kukubali kushindwa! Ukijua hivyo huwezi kukata tamaa kirahisi! Utajua unapoelekea! Utajua watu wakuambatana nao! Utajua ni vitu gani vya Kusoma! Mnyama wa kawaida hua anawaza vitu viwili tu…
HATUA YA 23: Unataka kwenda Mbali au Unataka Kufika Haraka?
Kuna msemo mmoja unasema kwamba “Kama unataka kufika haraka nenda/tembea mwenyewe. Kama unataka kufika mbali usiende peke yako nenda pamoja na wengine. “If you want to go quickly, go alone. If you want to go far, go together.” Ukienda peke yako Hutafika mbali, hutaenda mwendo mrefu utachoka. Kama safari yako ni ndefu usichague kwenda peke…
HATUA YA 22: Unacho cha Kupoteza?
Katika Maisha kuna mambo mengi sana huwa yanajitokeza na yanatufanya tuwe na hali za furaha au wakati mwingine hasira. Juzi wakati nasafiri kwenda Mwanza, kwenye bus kulikuwa na mtu alilipa akaa kwenye siti mbele ya safari akaja kuambiwa ilikuwa na mtu tayari yupo kituo cha mbele hivyo asimame. Pale ndani ya gari kukatokea mabishano makubwa…
HATUA YA 46: Ukweli Utakuweka Huru.
Kuna msemo mmoja unasema ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu. Walisema hivi kwa sababu ukidanganya halafu ukasahau ulichodanganya huwezi kuwa huru. Ukidanganya mara ya kwanza itakubidi udanganye mara ya pili. Uongo ni tabia mbaya sana ndio maana ulipokuwa mdogo ulichapwa sana pale ulipodanganya. Ukweli Utakuweka Huru kwa sababu huna haja ya kukumbuka ulichokisema. Mara zote unapokuwa…
HATUA YA 21: Tafuta Muda Mzuri na Wewe Peke Yako.
Ni Mara ngapi umekuwa ukiwapa watu muda wako? Ni mara ngapi umekuwa ukivipa vitu vya namna mbalimbali kwenye Maisha yako? Umekuwa ukitumia muda mwingi na Tv au marafiki lakini ukasahau kutumia muda na wewe mwenyewe. Umekuwa unatumia muda mwingi kazini kwako na kwenye shughuli zako nyingine lakini hupati nafasi ya kukaa na wewe pekee…