Hapo ulipo sasa usipadharau na kujiona upo nyuma sana. Kuna wengi sana wanatamani wafikie HATUA uliyofikia wewe. Kuna wengi wanajifunza kwa HATUA uliyofikia leo. Hata kama huoni wanaokupongeza kuna watu wanajifunza mno juu ya kile unachokifanya. Ninasema hivi Kwasababu inawezekana umekata tamaa na kujiona uko chini na wakati Mwingine kutokujali kile ulichonacho sasa. Kijali sana…
All posts in HATUA ZA MAFANIKIO
HATUA YA 20: Andika Historia.
Kila hatua unayopita hakikisha huachi hivi hivi, Hakikisha uneacha alama. Ni changamoto unapitia Hakikisha haikuachi hivi bure, utoke na cha kujifunza, Hakikisha Unatoka na hadithi Nzuri ya kuwaeleza watu. Maisha yetu yamefungwa kwenye muda, kadiri tunavyotumia muda ndio tunavyomaliza kuishi. Kila unachokifanya Hakikisha kinaacha alama. Watu unaokutana nao Hakikisha unawaacha wakiwa wa tofauti. Hakikisha unawaachia kitu…
HATUA YA 2: Unahitaji au Unajionyesha?
Nunua kitu Kwasababu unakihitaji sio kwa ajili ya kuwaonyesha wengine kwamba una uwezo wa kipesa. Tatizo kubwa linalotusumbua ni kwamba tunafanya mambo ili watu watuone. Mtu ananunua mavazi ya gharama sio Kwasababu anayahitaji bali ni ili watu wajue ana uwezo wa kipesa. Mwingine ananunua gari jipya ili watu waone sio Kwasababu ya mahitaji yake. Ukiwa…
HATUA YA 19: ASILI HAIBADILIKI.
Mojawapo ya vitu ambavyo havitaweza kubadilishwa ni vile ambavyo aliviumba Mungu. Lakini kila alichogundua mwanadamu unaweza kufikiri namna ya kukiboresha. Mwanadamu ukisema umuongezee kiungo kingine unaharibu mfumo mzima au hawezi kuwa sawa na wanadamu wengine. Huwezi kubadili chochote kinachotokana na asili. Waliojaribu kutuletea vitu ambavyo ni vya asili wakajaribu kurekebisha vinaleta madhara makubwa kwenye Maisha…
HATUA YA 1. Kupiga Hatua Kuna Gharama.
Kwenye safari yetu ya mafanikio kuna vitu vingi tunafanya ili tusonge mbele kila wakati. Ili mtu atoke sehemu moja aliyokuwepo na kusogea mbele anahitaji kulipa gharama. Sio kitu kirahisi kama unavyoweza kufikiri ndio maana sio wote wanaweza. Watu wengi huingia kwenye biashara au huanza vitu vipya na kutegemea matokeo bila kulipia gharama yeyote. Kama ilivyo…
HATUA YA 18: Usiishie Njiani.
Heri Ya Mwaka Mpya. Nina neno moja tu kwako mwaka huu wa 2017. #USIISHIE NJIANI. Yapo mengi sana Ulianza mwaka jana ukaweka malengo makubwa lakini ukaishia njiani. Mwaka huu sio wa kuishia njiani. Mwaka huu ni wa kumaliza ulichokianza. Mwaka huu ni wa kufikia mafanikio makubwa. Mwaka 2017 ni wa kwako wa Kupiga hatua. Mwaka…