Mtoto mdogo ndio binadamu pekee ambaye kile anachokifanya unaweza kuamini anakimaanisha kabisa. Hii ni kwasababu mtoto anakuwa hajajua chochote juu ya ukweli wala uongo, hajui kudanganya wala kuficha kitu. Mtoto mdogo ana Maisha yasiyo na hila ndani yake, anaishi kwa uhuru mkubwa kuliko binadamu wengine ambao tayari tumeshaingiza chachu ndani yetu. Kiwango hiki ndio kiwango…
All posts in HATUA ZA MAFANIKIO
HATUA YA 369: Usiuze Utu Wako.
Katika Muda mchache ambao nimekuwepo hapa duniani, kuna aina ya watu mbalimbali ambao nimeshakutana nao. Kuna aina ya tabia ambazo nimeziona zimekuwa zinanishangaza sana na wakati mwinginze zimekuwa zinasikitisha sana. Kuna aina ya tabia ukiwa nazo unaweza kujikuta umeuza utu wako na ukakosa kabisa umiliki wa Maisha yako. Wapo watu wengi ambao ninawafahamu wamekuwa na…
HATUA YA 368: Wewe Unasemaje?
Unaweza kukaa kwenye jamii ambayo haikuelewi kutokana na matendo yako au yale ambayo unayanena juu yao. Unaweza kukaa na marafiki ndugu au hata wazazi wasioelewa kusudi la wewe kuwepo hapa duniani. Kila mmoja anaweza kukupa tafsiri yake kulingana na uwezo wake wa kuelewa. Kitu cha muhimu sana sio vile watu wanavyosema juu yako bali ni…
HATUA YA 367: Kama Sio Sahihi Usifanye na kama Sio Kweli Usiseme.
Jambo lolote unalotaka kufanya lazima uwe na muda wa kujiuliza faida na hasara ya jambo lenyewe katika Maisha yako na ya wengine. Karibu kila jambo ambalo utafanya leo liwe baya au zuri linagusa Maisha ya wengine inawezekana ni moja kwa moja au sio moja kwa moja. Kwa kupitia matendo yako kuna Maisha ya wengi unayagusa,…
HATUA YA 366: Hakuna Hali Yeyote Inayodumu Kwenye Maisha Yako.
Maisha ni muunganiko wa matukio ya aina mbalimbali ambayo yanaendelea kila siku. Kuna nyakati utakuwa na furaha sana na kila unalolifanya linaleta matokeo yale uliyokuwa unayataka. Kuna nyakati mambo yatakuwa ni mabaya changamoto nyingi na utatakiwa uwe unawaza sana. Unachotakiwa kutambua ni kwamba yote hayo ndio Maisha. Haujawahi kuambiwa kwamba Maisha yatakuwa ni marahisi na…
HATUA YA 365: Hata Ukifika Mbinguni Ukarudi Bado Kuna Ambao Hawataamini.
Katika Maisha yako usikubali kuwa mtumwa wa kufanya vitu ili watu wakuamini au wakuthamini au wakukubali. Chochote kile unachokifanya sababu ya kwanza inatakiwa kuwa ni moyo wako uwe unapata furaha, sababu ya pili iwe ni kuna Maisha ya mtu unayasababisha yawe bora. Haya mengine yote ambayo yanakuja huku Njiani kama kusifiwa, kujulikana sana, kupongezwa, kupewa…