Inawezekana unafanya vizuri sana lakini hupati matokeo mapya mambo yanakuwa yale yale kwasababu unafanya kwa mazoea. “Hatufanyi vitu vya tofauti, tunafanya vitu vilevile lakini kwa tofauti” Kama unachokifanya kuna mtu mwingine anaweza kukifanya kabisa yaani sawa sawa na wewe ujiangalie vizuri sana. Inawezekana biashara moja wakaifanya watu wengi na baadhi yao wakapata matokeo bora yaani…
All posts in HATUA ZA MAFANIKIO
HATUA YA 59: Fanya Sasa.
Linalowezekana Kufanyika Leo Lisingoje Kesho. Pamoja na kwamba unakuwa na vipaumbele vyako vya maisha lakini siku zote linapojitokeza jambo ambalo linatakiwa kufanyika sasa hivi lifanye sasa hivi kwani kadiri unavyoahirisha ndio unajitengenezea mambo mengi huko baadae ya kufanya. Kuna changamoto unapitia sasa hivi zinatokana na vitu ulivyovipuuzaga huko nyuma kwasababu zako binafsi. Kuna ugonjwa unaumwa…
HATUA YA 57: Mafanikio ni Hatua
Inawezakana ulikua hujatambua hili na ukajikuta unapoteza nguvu yako ya kwenda mbele zaidi.Mafanikio sio kitu ambacho unataka kukikamilisha bali ni hatua ambazo unazifikia kila siku. Kadiri unavyoweza kupiga hatua ndio tunahesabu hayo ni mafanikio. Kama utachanganya katika ufahamu wako mafanikio na hatma utajikuta unakosa furaha na wakati mwingine kukata tamaa. Rafiki yangu ngoja nikwambie ukishindwa…
HATUA YA 56: Kama Upo Hapa Upo Sehemu Sahihi….
Kuna wakati mtu unapitia changamoto hadi unajiuliza hivi nafanya kitu sahihi kweli?Unapitia magumu hadi unafikiri labda unakoelekea siko kwenyewe. Leo nataka nikwambie haijalishi ni changamoto gani unapitia, haijalishi ni ugumu gani unapitia. Kama unachokifanya ndio kinaupa moyo wako utoshelevu kuliko vitu vingine vyovyote endelea kufanya upo sehemu sahihi.Kama unachokifanya ndio kinakupa furaha ya kweli hapo…
HATUA YA 54: Unamhitaji Mtu Huyu.
Tupo kwenye ulimwengu ambao watu wanafanya mambo wenyewe bila kupata mtu wa kuwaongoza hivyo hupelekea watu kukosea. Vilevile watu hukosa mtu wa kuwashauri wakati wanapopitia magumu na hivyo hukata tamaa haraka. Unamhitaji mtu wa kukuonya pale unapokosea. Unahitaji mtu wa kukuongoza kuelekea kwenye ndoto na maono yako. Unahitaji mtu ambae anafuatilia kwa karibu kile unachokifanya…
HATUA YA 51: Kuna Tatizo Una Tatua?
Katika zama hizi za sasa kila unachokifanya kuna mwingine anakifanya. Kama hakuna basi muda si mrefu wataanza kukifanya hasa wakiona kuna matunda. Ni muhimu sana kujua sehemu uliyopo kama ni sahihi kwako au lah! Unaweza kukutana na watu wengi ambao watakuonyesha vitu vingine vizuri vya kufanya zaidi ya kile unachokifanya sasa hivi. Watakuonyesha ni jinsi…