HATUA YA 65: Watu Wanatafsiri Walivyoelewa

Katika maisha tunafanya mambo mengi sana pamoja na maamuzi mbalimbali.   Kitu kimoja ambacho huwa tunakosea ni kuwalazimisha watu watuelewe.   Mara nyingine unaweza kujikuta unashindwa kufanya mambo fulani kwasababu unahofia watakuelewaje.   Leo nataka utambue kwamba huwezi kumridhisha kila mtu. Huwezi kumfanya kila mmoja akuelewe. Wakukuelewa watakuelewa tu. Ambao wataona makosa wapo wengi sana.…

HATUA YA 64: Unapojikwaa…..

Mara nyingi tunapitia changamoto mbalimbali kwenye maisha na tunapofikia kwenye hali hizo wengi wetu badala ya kuendelea mbele tunabaki palepale. Unapojikwaa jifunze kutembea vizuri lakini usikwame kwenye ile sehemu uliyoangukia. Safari bado inaendelea hivyo kama utabaki unaendelea kutazama kisiki utapoteza muda wako. Hakuna namna ambayo utaishi bila ya changamoto cha msingi ni kujifunza ili usije kujikwaa…

HATUA YA 63: Kuna Mtu Alifanya…..

Chochote unachokifurahia hapa duniani ambacho sio cha asili, ni matokeo ya binadamu mwenzako aliefanya kazi kwa bidii. Kila siku kuna watu wanafikiri ni kwa jinsi gani waendelee kurahisisha maisha yetu kwa kupitia ugunduzi wa aina mbalimbali. Kazi unayoifurahia sasa hivi na mshahara mzuri unaopokea kuna mtu alifanya kazi kwa bidii kukuza hiyo kampuni hadi wewe…

HATUA YA 62: Maisha Ni Uchaguzi

Vile ulivyo sasa au kile kinachoendelea kwenye maisha yako sasa hivi kwa namna moja ama nyingine ulichagua mwenyewe. Kuna uchaguzi ulifanya na ukakuletea matokeo unayopata sasa hivi. Ulichagua kutokuwa mwaminifu ndio maana mahusiano yako na mwenzako yakavunjika. Ulichagua kutokusoma vitabu ndio maana huna maarifa ya kutosha juu ya kile unachokifanya. Ulichagua kwa namna moja ama…

HATUA YA 61: Ukianza Siku Yako Hivi Unaiharibu…

Kwa kawaida Akili ya mwanadamu muda wa asubuhi inakuwa na nguvu sana na uwezo mkubwa wa kufikiri. Kama una kazi ngumu ukizianza asubuhi unajikuta umeweza kuzimaliza kwa haraka sana. Kwa kawaida unashauriwa wakati wa asubuhi ndio mzuri kufanya zile kazi ambazo ni nzito au zinazochosha akili yako. Hii itakuwezesha wewe baadae ukiwa umechoka umalizie na…