HATUA YA 110: Tua Mizigo Hii Uwe Huru 2.

Habari Rafiki, leo tena tunatazama baadhi ya mizigo mingine ambayo inaweza kuwa sababu yaw ewe kushindwa kusogea mbele.  Yapo mambo mengi sana yanatusonga kwenye Maisha lakini kiukweli hayana umuhimu wowote kwani yanazidi kuturudisha nyuma. Mambo Yaliyopita. Mambo mbalimbali yaliyokwishapita kwenye Maisha yetu yanaweza kuwa mizigo mizito sana ambayo inatufanya tushindwe kusonga mbele. Inawezekana ulipitia mambo…

HATUA YA 109: Tua Mizigo hii Maishani Mwako.

Maisha yako yanazidi kuwa magumu sana kutokana na mizigo mingi uliyobeba. Kuna mizigo mingine haina umuhimu wowote kwenye Maisha yako. Wakati mwingine Maisha yako yanaweza kuwa magumu kwasababu ya mizigo mingi uliyoibeba kwenye akili yako na katika uhalisia. Marafiki wabaya. Hawa wanaweza kuwa mizigo mikubwa kwenye Maisha yako kama utashindwa kuwawekea mipaka. Marafiki hawa wanaweza…

HATUA YA 108: Muhimu: Siku Ya Leo Fanya Kitu Hiki

Habari ya leo ndugu yangu mpendwa. Ninamshukuru kwa kufika hii hatua ya 108 bila ya kuacha kuandika hata siku moja. Nafurahi na wewe kuendelea kuwa msomaji wangu wa kila siku. Ninaamini kabisa kuna vitu unavipata hapa na vinakusaidia sana kwenye Maisha yako. Tuendelee pamoja hadi tufikie mafanikio makubwa sana. Kila sehemu unayoifanyia kazi hakikisha hauishii…

HATUA YA 107: Mambo 2 ya Muhimu kwenye Biashara Yako..

Mara nyingi biashara inapokuwa inaanza inaakua na njia nyingi sana na nzuri za kumjali mteja. Ila kadiri inavyokuwa na kupata wateja wengi huanza kushuka taratibu kwenye kuwajli wateja na ubora wa huduma. Kama na wewe umeingia kwenye kundi hili upo hatarini kuua biashara yako mwenyewe. Hatari inakuja Zaidi pale kile unachokifanya wako wengine wanakifanya pia.…

HATUA YA 106: Vitu Hivi Vinakurudisha Nyuma…

Unafurahia kufanya vitu gani? Unajua kuna yofauti ya kufurahia kufanya vitu na kupenda kufanya vitu Fulani? Mtu anaweza kufurahia sana kulala hasa wakati wa asubuhi lakini anajua kabisa ni hatari kwa mafanikio yake. Mtu anaweza kufurahia kufuatilia habari zisizomhusu wala kumsaidia lakini anajua kabisa anapoteza muda. Halafu mtu huyo huyo ukimwambia kuhusu kusoma vitabu atakwambia…