HATUA YA 216: Uliza Maswali.

Tatizo la wengi na linasosababisha tunapotea katika vitu visivyoeleweka ni kutokuuliza maswali. Wewe kama mwanadamu tofauti yako na Wanyama wengine ni uwezo wako wa kufikiri. Sasa kama mtu atakuja akasema kitu na wewe ukakifuata tu bila ya kujiuliza na kitu hicho hukijui ni kipya kwako inakuwa rahisi sana kupotezwa. Mfano umekwenda hospitali kumwona Daktari usikubali…

HATUA YA 213: Unajionaje?

Haijalishi watu watasema nini juu ya Maisha yako, haijalishi wataongea nini kinachojalisha ni mwitikio wako kwenye yale maneno yao. Haijalishi mtu amekutukana matusi makubwa kiasi gani kinachojalisha ni wewe umepokea kwa mtazamo upi. Vile unavyojiona wewe ina nguvu kubwa sana kuliko hata watu wanavyokutazama. Haijalishi watakusifia kiasi gani au kukukosoa kiasi gani kama wewe mwenyewe…

HATUA YA 211: Hakuna Tena Wa Kukuchapa.

Ulipokuwa mdogo kuna mambo ulikuwa ukifanya kinachokuja kufuata ni viboko.Mfano ukikutwa umepanda juu ya mti,  umegusa vitu ambavyo uliambiwa usiguse. Na mengine mengi unayokumbuka. Sasa wakati huu umekuwa mtu mzima usikubali kuendelea kuwa na mtazamo ule ule wa kitoto wa kuogopa watu.  Unajua Ulipokuwa mtoto ungeachwa bila ya kuchapwa inawezekana ungegunduaga mambo mengi sana. Lakini…

HATUA YA 209: Hii Ndio Siri ya Kutoingia Kwenye Madeni.

Inawezekana Umekuwa Mtumwa wa madeni na hayaishi kila siku unajikuta unatengeneza madeni mapya. Suluhisho sio kuwa na pesa nyingi bali ni kuwa na nidhamu. Kwasababu hata ukiwa na pesa nyingi kama una tabia inayokuingiza kwenye madeni utajikuta unaendelea nayo kila wakati. Usinunue kitu chochote ambacho Hukupanga. Kitu chochote unachokutana nacho njiani kiwe kizuri kiasi gani,…

HATUA YA 208: Unatumiaje Kidogo Ulichonacho?

Kabla Hujawaza kupata laki tano ya kuanzia biashara anza kuonyesha uwezo wako wa kutumia elfu hamsini. Kama ukishindwa kujua utaitumiaje elfu hamsini hata laki tano utashindwa kuitumia vizuri. Watu wengi tumekuwa tunalalamikia tatizo la mtaji  lakini tatizo sio mtaji tatizo lipo kwenye akili yako. Ili uweze kupata kile kikubwa unachokitaka jifunze kutumia kidogo kilichopo karibu…