Haitakuwa Rahisi Lakini Inawezekana. Ndoto yako kutimia haitakuwa rahisi lakini inawezekana kutimia. Kinachotakiwa ni wewe kutambua kwamba inawezekana kutoka ndani yako. Inatakiwa wewe uamua kwamba japokuwa itakuwa ngumu, japokuwa kuna maumivu ni lazima ufikie ndoto yako. Mafanikio na ndoto yako sio kitu kidogo hivyo usifikiri unaweza kuyafikia kirahisi tu. Haijalishi itakuwa ngumu kiasi gani wewe…
All posts in HATUA ZA MAFANIKIO
HATUA YA 222: Kujitetea Hakubadilishi Ukweli.
Nilipokuwa mdogo nakumbuka ilikuwa unapoharibu jambo mama akirudi unakimbilia kusema mabaya ya wenzako waliofanya. Unasema hivi ili kujipunguzia adhabu ya kosa lako. Lakini ukweli ni kwamba bado viboko vinahusika hata kama utajitetea vipi na kuwasema wengine. Kwenye Maisha ya sasa bado inawezekana una tabia kama za mtoto huyu ambaye akisaharibu anakimbilia kuanza kujitetea kwa kusema…
HATUA YA 221: Jifunze kwa Mgahawa wa Maisha
Mimi binafsi ninapokwenda mgahawani kwa ajili ya kupata chakula au kinywaji nikifika nikashindwa kuhudumiwa vizuri hua ninaondoka. Kwasababu gani? Kwasababu kama huwezi kunishawishi ninunue kwanini nikupe hela yangu na hujafanya chochote cha ziada. Kwasababu mimi binafsi sijaichukua mahali kama unavyotaka kuichukua kwangu. Sasa Maisha nayo ni kama mgahawa, ni mgahawa ambao una kila kitu ambacho…
HATUA YA 220: Jifunze Kwa Kuku.
Yapo mambo mengi tunaweza kujifunza kupitia hayo kama tu tutaweza kuyatazama kwa jicho la kujifunza. Kama utashindwa kutazama kwa jicho la kujifunza utaendelea kuyaona mambo kama kawaida ulivyozoea kuona siku zote. Kuku siku zote baada ya kuangua vifaranga vyake anaingia katika majukumu ya ulezi wa vifaranga vyake. Anapaswa kuwalinda na Wanyama wabaya na ndege kama…
HATUA YA 217: Hiki Ndio Kinakuzuia Kufanikiwa.
Umeamua Kuyatafuta mafanikio lazima ukubali kujikana uache kuishi yule mtu wa zamani ambaye alikuwa hakuletei maendeleo. Huwezi kusonga mbele kama bado umeshikilia tabia zile zile za zamani, lazima ukubali kuaziacha ili upokee mabadiliko mapya. Huwezi kuotesha mbegu kwenye shamba ambalo halijafanyiwa usafi. Kubali kufanyia usafi kwenye Maisha yako ili upokee vitu vipya. Mbegu zinazooteshwa kwenye…
HATUA YA 215: Tatizo lako lipo Hapa.
Ni rahisi kukua umri lakini sio kiufahamu. Ni rahisi sana kukua kiumri kwasababu kila siku mpya unakuwa umeongezeka umri lakini kiufahamu unaweza kubaki palepale hadi uongeze kitu kipya kwenye ufahamu wako. Ni hatari sana kama utakaa kwenye mazingira yale yale, ukaendelea kufanya vitu vilevile, ukabakia unajua vitu vilevile. Utakua kiumri lakini kiufahamu utabakia pale pale.…