HATUA YA 244: Tenda Wema Nenda Zako.

Ubinafsi ni kile kitendo cha kutaka kupata wewe peke yako na wengine wakose. Kitendo cha kutokujali wengine na kujifikiria wewe mwenyewe. Kujitoa kwa ajili ya wengine ni kitendo cha kuwa tayari kugawana kile unachokipata na wengine au wakati mwingine kuwa tayari kukosa ili wengine wapate. Kama wewe ni mtazamaji wa picha za kivita unaweza kuwa…

HATUA YA 243: Ukichunguza sana Hutafanya.

Kama kuna kitu umeamua kukifanya unachotakiwa ni kuchukua hatua sasa na kuanza. Mara nyingi wengi wanasema nitaanza tu, lakini baada ya muda ukimuuliza vipi ile biashara umeanza? Umeshaanza kufanya kile kitu? Watakwambia hapana.   Unapotumia muda mwingi kukichunguza kitu utaanza kupata hofu na hofu itakuzuia wewe kuanza kuchukua hatua. Unapochunguza sana utaanza kuona kutokuwezekana na…

HATUA YA 242: Hatua Unazopaswa kuzifuata Upate Mwelekeo wa mzuri wa Maisha

Moja ya makosa ambayo unaweza kuyafanya kwenye maisha yako ni kutokujua ni wapi unakwenda. Kitu cha pili ambacho utakuwa unaendelea kukosea ni unapojua unataka kuwa nani halafu basi ikaishia hapo hakuna chochote unachokifanya kinachoelezea kile unachotaka kuja kuwa. Kitu cha tatu ni kutokuwa na malengo na mipango iliyoandikwa na unaifanyia kazi kila siku. wengi ukiwauliza…

HATUA YA 240: Tatizo Lipo Ndani Yako.

Nimekutana na watu wenye uwezo mdogo, wana kiwango kidogo lakini wanafanya mambo makubwa sana. Wapo ambao hawana elimu kubwa uliyonayo wewe lakini wamefika mbali sana. Kuna wengine hawana wazazi wazuri kama wako lakini wamepiga hatua kubwa sana. Kinachokufanya ubaki hapo ulipo ni wewe mwenyewe. Unajiona kwamba huwezi, unaogopa changamoto ambazo utapitia njiani.   Ni kweli…