Kuna msemo wa wahenga unasema ukiona vyaelea ujue vimeundwa. Yaani chochote kile unachokiona kimependeza kwa nje unatakiwa ujiongeze kwamba kuna watu tena inawezekana wasiojulikana wamekifanyia kazi kwa wakati usiojulikana hadi kikaanza kuonekana kwa nje ni kizuri. Sasa wewe kwa tamaa zako unataka ukipate kile ambacho wenzako wamekifanyia kazi kwa muda mrefu sana hadi ukaanza kuvutiwa…
All posts in HATUA ZA MAFANIKIO
HATUA YA 256: Dunia Inakuhitaji?
Ni vyema kujiuliza na kujijibu kama kweli dunia inakuhitaji uendelee kuwepo hapa duniani. Lazima ujiulize hivi siku ukiondoka ni wakina nani wataguswa sana na kifo chako? Ili ujue ni kwa kiasi gani unahitajika hapa duniani lazima utambue ni thamani gani unatoa kwa dunia. Ni vitu gani vinatoka ndani yako na vinaleta matokeo na mabadiliko hapa…
HATUA YA 255: Unataka Kwenda Hatua Nyingine?
Unataka Kwenda hatua ya juu Zaidi? Lazima ukubali kupitia mitihani ya kukupima kama unaweza kukaa kwenye hatua inayofuata. Kama hutaki kupita kwenye mitihani huwezi kupanda hatua nyingine. Kama hutaki kupimwa hutaweza kuingia kwenye hatua za juu Zaidi utabaki hapo ulipo kwa muda mrefu Zaidi. Ukiona unabaki sehemu moja muda mrefu kuna uwezekano kuwa unafeli mitihani.…
HATUA YA 254: Huwezi Kupokea Mabadiliko kwenye Akili ya Zamani.
Kama wewe ni mtumiaji wa simu na unatumia hizi apps najua utakuwa umekutana na kitu kinakwambia update. Maana yak update ni kama kuboresha au kuongeza kitu kipya kwenye ile apps ya zamani. Watengenezaji wa apps hizi wanakuwa wameweka mambo mapya ndani ya apps sasa ili uyaone na kuyatumia hayo mambo mapya au muonekano mpya lazima…
HATUA YA 253: Hizi Ndio Nyakati za Kujua Kwanini Ulianza Unachokifanya.
Kwenye maisha kuna nyakati huwa zinatufikia ambazo zinakuwa ni kipimo ambacho kinaonyesha ukweli wa makusudi yetu kwa yale tuliyokuwa tunataka au tayari tunafanya. Unaweza kukutana na changamoto kubwa kiasi kwamba ukafikia hatua za kusema kama hali ni hii basi sifanyi tena hiki kitu. Lakini ukweli unabaki pale pale kwanini uliamua kufanya? Kabla hujakata tamaa ni…
HATUA YA 252: Uko Hivyo Ulivyo Kwa Kuamua.
Wako waliopitia changamoto kubwa kuliko wewe lakini hawajakata tamaa. Wako ambao walipata hasara kubwa sana kuliko hyo ambayo unajitetea nayo lakini bado wakasonga mbele na sasa tunazungumzia mafanikio yao makubwa. Wako waliochwa na waale waliowapenda sana lakini hiyo haikuwa sababu ya wao kuacha kutimiza ndoto zao bado wakasonga mbele tu. Hiyo kwao haikuwa sababu kubwa…