HATUA YA 273: Ipo Sababu

Kila linalotokea kwenye maisha yako linatokea kwasababu usiwe mwepesi wa kulaumu au kulalamika wakati mwingine utajikuta unakosea. Kuna nyakati unaweza kuona umepatwa na mabaya Fulani kumbe sababu ya mabaya hayo ni kukuepusha na mabaya Zaidi. Unaweza kuona mahusiano yako yanapitia changamoto na misukosuko hadi yakavunjika kumbe Mungu alikuwa anakuepusha na aibu ambayo ingekupata huko mbele.…

HATUA YA 272:  Kama Umeamua Kwenda Nenda.

Kutazama tazama nyuma kumekuwa sababu ya wengi kugeuka na kurudi walipotoka. Wakati changamoto zimekuwa nyingi kwenye safari yako ndio wakati hasa wa kutazama mbele badala ya kule ulipotoka. Wakati kuna giza ndio wakati hasa wa kutafuta mwangaza. Wakati tumefika sehemu hatuoni njia ndio wakati wa kutafuta njia. Kinachowafanya wengi washindwe kufika popote ni kwasababu hakuna…

HATUA YA 271: Tabia Hii Inakuwekea Miiba mbele ya Safari.

Katika maisha kuna mambo tunafanya kwa kujua ama pasipo kujua na mambo hayo yanakuja kuwa miiba katika safari za mafanikio yetu. Ni vyema sana ukatambua unachokifanya sasa hivi kitaleta madhara gani baadae kwasababu ndiko unapokwenda. Usijisahau kwa chochote ulichonacho unakafikiri umeshamaliza safari. Waliomaliza safari ni marehemu peke yao. Popote ulipo sasa hivi upo kwenye safari,…

HATUA YA 270: Wanakupenda sana ila wanakuharibia Bila Kujua.

Kama ukipata tatizo lolote kwenye maisha yako kuna sehemu ukienda ukajieleza tu unaeleweka na tatizo lako linatatuliwa unaweza kufikiri kwamba upo sehemu nzuri sana. Ukweli ni kwamba upo sehemu ya hatari kuliko nyingine yeyote kwenye maisha yako. Ni rahisi sana mtu kupenda pale ambapo akipeleka matatizo yake yanatatuliwa. Ni hatari sana kama hayo matatizo ulipaswa…

HATUA YA 269: Huhitaji Kikubwa Sana.

Mara nyingi tunafikiri ili ufikie hatua kubwa kwenye maisha lazima uanze na mwanzo ambao ni mkubwa sana. Usifikiri kwamba ukiwa na vitu Fulani na Fulani basi ndio maisha yako yatakwenda vizuri. Kama umeshindwa kutumia rasilimali ulizonazo sasa hivi hata ukipewa kubwa bado utashindwa na unaweza ukaharibu badala ya kutengeneza. Uwezo wako unapimwa kwa namna ambavyo…

HATUA YA 268: Swali La Kujiuliza Unapojua Unachokitaka.

Kujua kile unachokitaka ni jambo la kwanza, kinachofuata ni kufahamu gharama ambazo unapaswa kulipa ili kufika pale unapotaka. Wengi wanaishia kwenye kujua wanachotaka na kukata tamaa baada ya kuambiwa gharama wanazotakiwa kulipa.   Ni vyema ukajiuliza maswali haya na ukapata majibu yake wakati unaanza safari yako. Unajua gharama gani unapaswa kulipa ili ufike unakotaka kwenda?…