Maisha Yako yaliyokwisha kupita ni kama kivuli nyuma yako. Sio kila mtu anaekutazama ataweza kuona kivuli chako labda awe alishakuwa nyuma yako. Unachotakiwa kujua ni kwamba kivuli hakiwezi kuondoka hasa unapokuwa kwenye mwangaza. Pamoja na kuwa kivuli chako kinaendelea kukufuata hakitakiwi kiwe sababu ya wewe kushindwa kusonga mbele. Ni kweli kuna vivuli vingine vinatisha sana…
All posts in HATUA ZA MAFANIKIO
HATUA YA 309: Hiki Ndio Kisasi Bora kwa Adui Zako.
Huwezi kuondoa chuki kwa kuchukia, kama mtu akikutendea ubaya wewe ukimtendea ubaya unakuwa huna tofauti na yeye. Huwezi kuzima moto kwa kuuongezea vichocheo vinavyoufanya uendelee kuwaka. “The best revenge is not to be like your enemy.” ― Marcus Aurelius, Meditations Mwanafalsafa huyu Marcus aliwahi kusema “Kisasi cha kweli ni kutokuwa kama adui Yako” Yaani watu wanaopambana kukuangusha…
HATUA YA 308: Maoni ya Watu Wengine Juu Yako.
Tumezungukwa na watu wengi ambao wanatutazama kwenye yale tunayofanya kila siku. Wapo ambao wanatupenda na wanatamani kuona tunafika mbali vilevile wapo ambao wanatuchukia tu na wanatamani siku zote kuona tunateseka. Ni vyema tu ukaelewa hilo kwamba kuna watu wa aina hiyo kwenye Maisha yako na kile ambacho unakifanya. Ukiweza kutambua hivyo utajua namna bora ya…
HATUA YA 307: Huu Ndio Uhuru Wa Kweli.
Uhuru sio kuamua kufanya unachokitaka bila kupangiwa au kusimamiwa na mtu yeyote. Endapo ingekuwa ni hivyo basi kungekuwa na uharibifu mkubwa kwasababu ya asili yetu wanadamu. Wanadamu tuna asili ya kutokutosheka na pia ukichanganya na wale walio na nia zisiozo nzuri unakuwa unatengeneza uharibifu Zaidi. Pamoja na kwamba unaweza kuwa na nguvu nyingi sana za…
HATUA YA 306: Vinavyotokea Vyenyewe.
Vitu vinavyotokea Vyenyewe Kwenye Maisha yako mara nyingi ni vitu ambavyo Huvihitaji, na wala havina mchango chanya kwako, ni kama magugu ndani ya shamba. Kutarajia vitu vitokee kwenye Maisha yako na hujaweka juhudi zozote basi ujue kitakachotokea hakina tofauti na magugu. Usipojitoa kupata kile ambacho unakitaka utajikuta siku zote matokeo unayopata sio yale ambayo unatamani…
HATUA YA 305: Wakati Wako Upo.
Haijalishi unapitia hali gani sasa, unapaswa kujipa moyo na kujitia nguvu kwasababu wakati wa wewe kufanikiwa na kuinuka kwenda viwango vingine upo. Unaweza kupambana sana na kutumia kila njia ambazo unafundishwa na unazosoma kwenye vitabu lakini ukajishangaa kwamba hakuna mabadiliko yeyote. Unapaswa kuendelea kujipa moyo kwamba hautabaki kama ulivyo milele. Asubuhi yako inakuja usitishwe wala…