HATUA YA 334: Ukitaka Kuwa Mkubwa wa Wengine Kubali Hiki..

Kanuni ya kuwa Mkubwa wa wengine siku zote ni kutumika. Hakuna bosi alieweza kuajiri maelfu ya watu kwenye kampuni yake kama hakutoa muda wake akitumika hadi akafikia uwezo wa kuajiri. Hakuna aliefikia mafanikio makubwa na kujulikana na wengi kama hakutoa nguvu zake katika kuonyesha ule uwezo uliokuwa ndani yake. Hata kama una sauti nzuri ya…

HATUA YA 333: Usipoteze Muda Kwenye Kitu Hiki Kabisa.

Tunayaelewa mambo kulingana na uwezo wetu wa kufikiri na namna mitazamo yetu ilivyo. Kama ni hivyo basi utakuwa ni upotevu wa muda usio na msingi kabisa kama utakaa kwenye kundi la watu ukibishania, mpira, siasa, dini, au kitu kingine chochote. Kila mtu anaweza kutetea kile alichokiamini, sio rahisi ubadilishe Imani ya mtu kwa maneno matupu…

HATUA YA 332: Unajijengea Ukuta Au Unafungua Njia?

Katika Maisha yetu ya kila siku na vitu tunavyofanya kuna kitu ambacho tunatengeneza. Vile unavyoishi Maisha yako kuna picha watu wanaijenga kuwa wewe ndio hivyo ulivyo. Vile unavyoongea kuna picha watu wanajenga kwenye akili zao kwamba wewe ndio hivyo upo. Kama unaongea maneno ya hovyo picha itakayojengeka ni kwamba wewe ni wa hovyo. Kama utakuwa…

HATUA YA 331: Ukielewa Hili Huwezi Kuwa na Maumivu Ndani ya Moyo.

“We suffer more often in imagination than in reality” ― Seneca Mara inaweza kuwa jambo dogo sana limetokea mahali lakini kwa kupitia fikra zetu tukajikuta tumekuza lile jambo na kuendelea kupata maumivu makubwa. Mwanafalsafa Seneca anasema tunateseka Zaidi katika vitu tunavyovifikiria kuliko vile vitu halisi. Mfano mdogo ni pale umempigia mtu simu hakupokea au akaikata unaweza…

HATUA YA 329: Ni Majukumu Yako, Hakuna Haja ya Kuwatangazia watu.

Mtoto mdogo anapofanya jambo la tofauti na alilozoea kufanya na akafanikiwa mara nyingi hupenda kwenda kwa mzazi wake na kumwonyesha huku amejawa na furaha sana. Inaweza kuwa ni mtihani shuleni au majukumu aliyopewa kutekeleza. Lakini tukija kwenye uhalisia kufaulu mtihani shuleni kwa mtoto ndio jukumu lake hasa. Anakwenda shuleni kusoma na kujifunza ili afaulu. Tunapokuja…