HATUA YA 340: Vitu Hivi Viko Sambamba Siku Zote.

Huwezi kusema unataka mwili wenye misuli bila ya mazoezi magumu na mazito. Huwezi kusema unataka mtoto lakini hutaki kubeba majukumu ya kupata mtoto. Maumivu, kukataliwa, kupingwa, kusemwa vibaya, kuonekana umechanganyikiwa ni dalili zinaonyesha kwamba kile unachokifanya kina matokeo makubwa sana na hakijawahi kufanywa na wengine. Dalili ya kwanza ya kujua kule unapoelekea ni kwa namna…

HATUA YA 339: Ukisubiria Nafasi Itokee, Wenzako Wanatengeneza Nafasi.

Kwenye Maisha unapaswa uweze kutofautisha kati ya vitu ambavyo unatakiwa uvifanye vitokee na ambavyo unatakiwa usubiri vitokee kwa uweza utokao juu. Ukishindwa kuvitofautisha hivi unaweza kukuta unateseka sana kwenye mambo ambayo ulipaswa kufanya mwenyewe. Unapoteza muda kwenye vitu ambavyo havipo kwenye uwezo wako wa kuvifanya vitokee. Ukiwa na vipaji vizuri vya uchoraji ukachora picha ukaziweka…

HATUA YA 338: Jua Kusudi Lako, Ili Usiteseke na Majira ya Wengine.

Kama tunasema kila binadamu ana upekee wake basi ni kama zilivyo mbegu za mimea mbalimbali. Kila mbegu ina muda wake wa tofauti katika kuonekana imeanza kuchipuka kutoka ardhini. Ukipanda mahindi au maharage unaweza kutegemea kuuona mmea umeanza kuchipuka siku ya tatu hadi saba. Lakini tukija kwenye mimea mingine kuna ambayo hupita muda mrefu sana hadi…

HATUA YA 337: Hakuna Kinachotokea Bila Ya Sababu Hata Kama ni Kibaya.

Unapoona mabaya yamekuja kwako usiwe mwepesi wa kulalamika bali penda kujiuliza maswali. Penda kudadisi ni wapi umekosea au ni kitu gani unapaswa kujifunza. Umeingia kwenye mahusiano na mtu na mkajikuta mnashirikiana kwenye mambo mengi kwa pamoja. Maono yenu mkaweka pamoja, na baadhi ya mambo mkaanza kufanya pamoja. Mnakuza vitu pamoja hadi mnafikia Hatua ya kubwa…

HATUA YA 336:  Kwenye Dunia Unayoweza Kuwa Chochote Unachotaka.

Kwenye dunia hii ambayo kila unachotaka kuwa unaweza kuwa ni vyema ukachagua kuwa mwema. Hii ndio njia pekee ya kwanza kuonyesha wewe ni binadamu. Mtu anapofanya jambo baya la kikatili kuna usemi hutumika “amefanya jambo la kinyama sana” yaani maana yake wewe kama binadamu tofauti yako na Wanyama wengine ni ule utu ulioko ndani yako.…

HATUA YA 335: Hamasa Yako ya Ndani Inaletwa na Nini?

Kila mtu kulingana na kile anachokitaka kuna namna anakuwa na hamasa ndani yake. Swali la kujiuliza ni kitu gani hasa kinakupa hamasa? Kitakachoamua udumu kwenye maamuzi uliyofanya ni kile chanzo cha hamasa yako. Kitakachoamua uweze kushinda changamoto ni kile chanzo cha hamasa yako ya ndani. Kama ndani yako hakuna kitu kinachokusukuma kufanya kama vile vya…