Kwa lolote lile ambalo unapitia kwenye maisha yako sasa hivi. Liwe zuri au liwe baya ni vyema kuwa na muda wa kujiuliza swali kwa yote hayo unayopitia ni yapi unajifunza? Kwa yote yanayoendelea kwenye maisha yako ni somo gani unaondoka nalo? Usikubali tu kuishia kuumia au kufurahi bila kuondoka na somo lolote. Ukiwa mtu ambaye…
All posts tagged chukua hatua
#USIISHIE_NJIANI: Hali Mbaya Uliyonayo Inasababishwa na Hiki
Leo jioni nikiwa nazishika ndevu zangu ghafla katika fikra yakanijia maneno ambayo niliambiwa miaka karibia kumi iliyopita. Kuna mtu mmoja aliniambia “wewe ukiwa na ndevu utakuwa mbaya sana”. Nikabaki najiuliza kwanini haya maneno yamekuja sasa hivi wakati nashika ndevu? Mbona ni muda mrefu sana umepita na nilishayasahau kabisa? Nikagundua kwamba maneno uliyonenewa na watu yanabaki…
#USIISHIE_NJIANI- Jawabu la Unachokitaka ni Hili hapa.
Penda kujipa muda wa kusubiri matokeo unayoyataka wakati unayafanyia kazi. Bahati mbaya hatuna kipimo maalumu cha muda ili uwe na uhakika wa unachokisubiria. Kama mwanamke amebeba ujauzito inafahamika kabisa ni baada ya miezi tisa atajifungua. Na endapo itatokea tofauti na hapo muda ukizidi tunaanza kupata wasiwasi. Kwenye mafanikio hakuna mahesabu ambayo yapo na uhakika kabisa…
#USIISHIE_NJIANI: HOFU YA KUTOKUJUA.
Habari rafiki, siku yako umeanzaje. Siku zote mtu anakosa ujasiri hasa pale anapokuwa na taarifa chache kwenye kile anachokifanya. Mfano unaweza kuogopa kuanza biashara kwasababu tu ya kutofahamu mambo ya muhimu juu ya biashara. Ili uweze kuishinda hofu hii unapaswa kujifunza vitu Zaidi kwenye kile ulichoamua kukifanya. Hii itakusaidia wewe kuwa na taarifa za kutosha…
#USIISHIE_NJIANI: DUNIA INAKUTAZAMA.
Wakati unaanza ulianza kwa mbwembwe na kelele nyingi, ulipenda kila mmoja ajue kwamba unaanza biashara au kipaji chako. Kuna waliokupinga, waliokukatisha tamaa, waliokutia moyo, waliosema umechagua njia sahihi. Naomba nikukumbushe kwamba bado dunia inakutazama yale uliyosema utafanya bado wanaakuchungulia kama ni kweli yatatokea au lah. Kama utakubali kukata tamaa utakuwa umewathibitishia wale waliosema kwamba huwezi,…
HATUA YA 1. Kupiga Hatua Kuna Gharama.
Kwenye safari yetu ya mafanikio kuna vitu vingi tunafanya ili tusonge mbele kila wakati. Ili mtu atoke sehemu moja aliyokuwepo na kusogea mbele anahitaji kulipa gharama. Sio kitu kirahisi kama unavyoweza kufikiri ndio maana sio wote wanaweza. Watu wengi huingia kwenye biashara au huanza vitu vipya na kutegemea matokeo bila kulipia gharama yeyote. Kama ilivyo…