#USIISHIE_NJIANI: Hali Mbaya Uliyonayo Inasababishwa na Hiki

Leo jioni nikiwa nazishika ndevu zangu ghafla katika fikra yakanijia maneno ambayo niliambiwa miaka karibia kumi iliyopita. Kuna mtu mmoja aliniambia “wewe ukiwa na ndevu utakuwa mbaya sana”. Nikabaki najiuliza kwanini haya maneno yamekuja sasa hivi wakati nashika ndevu? Mbona ni muda mrefu sana umepita na nilishayasahau kabisa? Nikagundua kwamba maneno uliyonenewa na watu yanabaki…

#USIISHIE_NJIANI: MAMBO YA KUZINGATIA ILI USIISHIE NJIANI.

Furahia kila wakati unaopitia lakini usijisahau kuwa upo safarini. Unapokuwa safarini tena kwenye safari hii ya maisha kuna mengi utakutana nayo njiani usikubali kubakia sehemu moja kwasababu kuna mazuri umekutana nayo. Furahia hayo mazuri lakini usikubali yawe sababu ya wewe kubakia hapo. Kwenye maisha jifunze kuchagua kwani kile unachochagua kinaonyesha jinsi wewe ulivyo. Marafiki ulionao,…

#USIISHIE_NJIANI-  Jawabu la Unachokitaka ni Hili hapa.

Penda kujipa muda wa kusubiri matokeo unayoyataka wakati unayafanyia kazi. Bahati mbaya hatuna kipimo maalumu cha muda ili uwe na uhakika wa unachokisubiria. Kama mwanamke amebeba ujauzito inafahamika kabisa ni baada ya miezi tisa atajifungua. Na endapo itatokea tofauti na hapo muda ukizidi tunaanza kupata wasiwasi. Kwenye mafanikio hakuna mahesabu ambayo yapo na uhakika kabisa…

#USIISHIE_NJIANI- Kujionyesha na Uhalisia.

Haina maana yeyote kama watu watajenga picha kubwa kwako kutokana na namna unavyopenda kujionyesha halafu uhalisia ukawa ni tofauti kabisa. Ni vizuri sana ukaishi vile unavyopenda lakini ni vyema ukakubali kulipa gharama za hayo maisha kwanza ndipo uje kufurahia baadae. Ni kichekesho sana kama utakuwa unatamani watu waone unaishi maisha mazuri wakati kwa ndani unateseka…