SURA YA 438; Sio Kama Unavyofikiri.

Kuna watu ukiwatazama kwenye mitandao ya kijamii unaweza kutengeneza picha Fulani ya Maisha ambayo wanaishi na ukaanza kujiona wewe si kitu kabisa. Ukaanza kuona wewe umeachwa sana nyuma na wenzako Maisha yao yako viwango vya juu sana. Ukweli Rafiki ni huu inawezekana ni kweli kabisa wanachoweka mitandaoni ni Maisha yao, sasa wewe ukiumia kuna kitu…

SURA YA 436; Usiwe Kigeugeu.

Ukishajua unachotaka hupaswi tena kuwa na hofu yeyote kwamba itakuaje. Leo unasema unataka hiki kesho ukiona wenzako wamefanya kitu kingine wakapata matokeo ya haraka unataka kuacha ili na wewe ukafanye kama wao. Wewe endelea mbele kwenye kile ambacho ulichoamua kukifanyia kazi na ukiweka juhudi za hali ya juu. Usiogope ugumu maana hakuna sehemu ambayo ni…

SURA YA 435; Sio Bahati Mbaya.

Usimcheke mtu kwa hali yeyote anayopitia kwenye maisha yake. Hata kama imechukua muda mrefu usinene mabaya yeyote juu yake. Kuna nyakati unapitia bila kujua, kumbe ni Mungu anakuandaa ili uweze kuwa vizuri sehemu anayotaka akupeleke (kwenye kusudi lake). Musa hakwenda kuishi kwa Faraoh ili ale bata, au asiuwawe. Alipitia kule ili ajifunze uongozi ili aje…

SURA YA 434; Ukifika Katikati Unajikuta Umeshaanza Kingine.

Asilimia kubwa ya watu hupanga malengo mengi wanapoanza mwaka lakini inapofika katikati ya mwaka unawakuta watu wale wale wameshaacha kabisa vile vitu walivyopanga kufanya na kufanya vingine vipya ambavyo hawakupanga kabisa. Hii inasababishwa na kukosa hamasa, kukata tamaa kidogo kidogo na kujikuta umeanza kuvutiwa na jambo jingine ambalo umelisikia. Unaweza kuanza malengo yako kwa hamasa…

SURA YA 433; Ni Matatizo Yako.

Ukisema huna mtaji wa kuanza biashara, hayo ni matatizo yako hakuna anaehusika sio mzazi wala serikali. Ukisema mambo ni magumu kwako hayo pia ni matatizo yako Rafiki, njia pekee ni wewe kutafuta suluhisho na sio kuwabebeshea wengine. Serikali haihusiki kwenye matatizo yako binafsi, unaweza kusema hapa kwamba kuna namna inahusika kwasababu mbalimbali ambazo unatoa lakini…