HATUA YA 43: Kitu Hiki Pekee Ndio Kinaweza Kukuzuia Kutimiza Ndoto.

Yapo mambo mengi sana yanaweza kukuzuia au kukurudisha nyuma kwenye kutimiza ndoto yako lakini hayana uwezo wowote wa kuamua ushindwe. Jambo lolote unaloona linakuzuia wewe iwe ni changamoto au maneno ya watu siku zote hua hayana nguvu yoyote. Nguvu ya wewe kuacha hutoka ndani yako. Usije kujitetea hata siku moja kwamba kuna watu walisababisha wewe…

HATUA YA 42: Tengeneza Picha.

  Bila picha hakuna mwelekeo. Bila  Picha hakuna maisha.  Bila picha utachukuliwa na kila kinachokuja.   Picha inakupa mwongozo, Picha inakupa vipaumbele. Picha inakupa uwezo wa kuchagua marafiki. Picha inakupa hamasa. Picha inakupa ujasiri. Picha inakupa uwezo wa kujieleza.   Kama huna picha ya maisha yako ya baadae utayumbishwa sana na mambo yanayoendelea duniani.  Kwenye…

HATUA YA 41: Usipofanya Hiki Hakuna Kitakachobadilika.

Kwenye Maisha yetu siku zote kila mtu anatamani mabadiliko, kila mmoja anatamani kupata vitu Fulani kwenye Maisha yake. Ili ubadili chochote kwenye Maisha yako lazima ukubali kuchukua hatua. Kama kweli Unakihitaji kitu utakitafuta. Na ukikitafuta kwa bidii utakipata. Mara nyingi unaweza kuonyesha hamasa kubwa sana ya kupenda mafanikio na unayazungumzia sana lakini hakuna unachofanya ili…

HATUA YA 40: Unaondokaje Duniani?

“Tukijifunza kuacha historia njema kwa kutenda mema katika maisha ya wengine itatuwezesha tuondoke duniani tukitabasamu na huku tukiwaacha wengi wakitokwa na machozi” Katika kitabu changu Kiitwacho Siri 7 za Kuwa Hai Leo  nimezungumzia juu ya kutengeneza historia mpya. Inawezekana umeshatenda mambo mengi mabaya kwenye maisha ya wengine kwa namna mbalimbali lakini kama bado upo hai…

HATUA YA 39: Huyu Ndie anahusika Kuyafanya Maisha yako Yafanikiwe.

Maisha magumu uliyonayo sasa, madeni sugu, Kipato cha chini na matatizo mengine yote uliyonayo kuna mtu mmoja pekee anahusika kuyatatua. Ukweli unatakiwa umfahamu mtu huyu ili uweze kukaa nae vizuri sana akuwezeshe kuondokana na shida ulizonazo. Kwenye Makala yetu ya leo utakwenda kumjua mtu huyu ambaye anahusika kabisa na ni jukumu lake kukufanya wewe ufikie…

HATUA YA 38: Nani Anafanya Unachokifanya?

Kwenye dunia hii hakuna kitu ambacho utakifanya uwe umeanza peke yako. Chochote unachotaka kukifanya kuna mtu alishakifanya au bado anaendelea kukifanya. Ni muhimu sana kufahamu ni nani anafanya kile unachotaka kufanya au unachokifanya. Nia ya kufahamu sio ili umjue mshindani wako hapana ni ujue nani wa kujifunza kwake. Ukifahamu mtu huyu au watu hawa wanaofanya…