Kanuni ya Umaskini ni kutumia Zaidi ya unachozalisha. Kama unataka kubakia kuwa maskini endelea kuwa na matumizi makubwa kupita uwezo wako wa kuzalisha. Kama wewe ni mkulima ukizoea kula Zaidi ya unachozalisha mwisho wa siku utakula na mbegu inayokuzalishia. Kama wewe ni mfanyabiashara ukizoea kutumia Zaidi ya unachopata utaanza kula mtaji. Kanuni ya mafanikio inasema…
All posts in HATUA ZA MAFANIKIO
HATUA YA 200: Pima Kazi Yako Hivi.
Leo ni siku ya 200 mfululizo tangu nimeanza kuandika. Unaweza kufikiri ni kitu rahisi lakini sio kitu rahisi maana ili uandike lazima ujilazimishe kufikiri sana. Sasa kama mtu ni mvivu kufikiri hawezi kuandika kila siku. Lakini ni kwambie siri iliyopo nyuma ya hizi hatua 200? Wakati naanza nilifika hatua kama ya 50 hivi wakajitokeza watu…
HATUA YA 199: Wasikilize Lakini Amua Wewe.
Kwenye vitu tunavyovifanya kila siku tunakutana na maoni ya wengine kila siku. Jambo la muhimu ni kwamba usikatae kupokea maoni ya watu. Kitu unachotakiwa ni kuyachuja na kuchagua yale ambayo unaona yanafaa kule unapoelekea. Usiruhusu watu wakufanyie maamuzi maana wewe ndie unajua unapoelekea. Usiwape wengine madaraka ya kuamua wewe uwe na baadae ya aina gani.…
HATUA YA 198: Ukikosa Vipaumbele.
Ukikosa vipaumbele huwezi kujua ni nani anastahili muda wako Zaidi ya wengine hivyo utakua unapoteza muda hata kwa watu wasio wa muhimu. Ukikosa vipaumbele huwezi kujua kipi ni cha muhimu Zaidi ya kingine hivyo utakuwa unafanya vitu hovyo hovyo tu. Ukikosa Vipaumbele utachukuliwa na kila kinachokuja mbele yako itakuwa ngumu sana kwako kufanya uchaguzi.…
HATUA YA 197: Tengeneza Mazingira.
Kuku anapotaka kutaga kwa mara yake ya kwanza lazima atafute sehemu nzuri na aitengeneze ili aweze kutaga vizuri. Kwa bahati mbaya sana kuku hana akili hivyo anaweza kujitafutia sehemu yeyote tu hata nje ya banda lake. Ila kwa mfugaji anaejua kitu anafanya lazima awaandalie kuku wake mazingira ya kutaga pale wanapohitaji kutaga. Kipindi Fulani kuku…
HATUA YA 196: Kuna Mahali Ulisababisha.
Mambo mabaya yote yanayotokea kwenye Maisha yako sio kwa bahati mbaya kuna mahali uliyasababisha yakatokea. Badala ya wewe kuchukua muda mwingi kulaumu na kulalamika jiangalie kwa upande wako unahusikaje kusababisha. Tuchukue mfano rahisi watu wawili wanagombana hadi kutaka kupigana, ukikaa na mmoja wapo ukamuuliza ilikuaje ataanza kumtupia lawama mwenzake. Lakini ukweli hadi wakafikia kugombana yeye…