Ukweli ni kwamba hakuna mtu asiyependa mafanikio, hata maskini kabisa anatamani sana atoke kwenye umaskini wake awe na mafanikio. Tatizo linakuja kwenye kile ambacho mtu anakifanya ili awe na mafanikio. Sasa cha ajabu ni kwamba watu wanafanya vitu kila siku lakini hawajui kama wanavyovifanya ni sahihi au lah. Leo nataka ujiulize swali hili la muhimu…
All posts in HATUA ZA MAFANIKIO
HATUA YA 387: Ukikosea Utapigwa..
Shule ya Sekondari niliyosoma kulikuwa na waalimu ambao nawakumbuka mpaka sasa. Mwalimu mmoja alisifika sana kwa kufundisha vizuri sana, Mwalimu mwingine alisifika sana kwa kuchapa viboko. Wote ni waalimu lakini mmoja ana sifa ya kazi yake na mwingine ana sifa ya kuchapa. Hapa kuna kitu cha kujifunza Rafiki wewe unataka sifa gani kwenye kile unachokifanya?…
HATUA 386: Ndoto Yako Inakuhamasisha?
Mhamasishaji wa Kimataifa Les Brown aliwahi kusema kwamba sio kuwa wtau hawana malengo watu wana malengo lakini ni madogo sana kiasi kwamba wanayatimiza haraka sana bila ya changamoto yeyote. Unapaswa kuweka malengo makubwa ambayo hata usipoyafikia basi yatakuwa yamekuwezesha ufike mbali sana. Ndoto yako inatakiwa iwe kubwa kiasi kwamba inakuhamasisha kuamka asubuhi na mapema uende…
HATUA YA 385: Ukitaka Kueleweka Acha Kutafuta Kueleweka.
Ukweli ni kwamba ukitafuta kueleweka utakuwa unawachanganya watu badala ya watu kukuelewa. Kitu ambacho unaweza kukifanya pekee ni kuendelea kufanya kile unachoamini, endelea kuwa wewe hata kama watu wanakupinga. Kutaka kueleweka na kila mtu ni kazi ngumu sana ambayo wengi walishashindwa. Ukianza kuishi kile unachokiamini kuna watu wengi wataendelea kukufuata kwasababu wataanza kuamini kile unachokifanya.…
HATUA YA 384: Unahitaji Kuwa na Watu Hawa Wa Muhimu.
Mafanikio yako yamebebwa na watu wengine. Ili uweze kufika mbali lazima uwajue watu ambao ni sahihi kwenye mafanikio yako. Pesa unazozihitaji zipo kwa watu sasa ni jukumu lako kujua ni watu hasa wanazo pesa zako. Na sio kuishia kujua tu ni lazima kwanza uwe umejua wewe una kitu gani ndani yako ambacho kitakuongoza kuwajua watu…
HATUA YA 383: Ni Haki Yako Lakini Lazima Uumie
Unajua kila kitu kizuri hapa duniani ni kwa ajili ya kila binadamu? Unajua kwamba hata wewe unastahili dhahabu, ndege, au chochote kizuri? Unajua kila ambacho umekuwa unakitamani kwenye akili yako ni sawa kabisa? Ni kweli ni haki yako, mafanikio ni haki yako, utajiri ni haki yako, kuwa mtu mkuu ni haki yako. Lakini sasa ili…