Kwa kawaida hakuna kitu kimoja unachoweza kufanya kikakufikisha kule unakotaka moja kwa moja. Hapa nikiwa na maana ya kwamba ukitaka kuvuna mahindi gunia mia unatakiwa upande mashimo mengi sana ya mahindi kwenye mashamba. Huwezi kutegemea shimo moja likuletee hayo mahindi hata kama utaweka mbolea ya kutosha, ukahakikisha hayaguswi na wadudu, bado shimo moja halitoshi kuleta…
All posts in HATUA ZA MAFANIKIO
HATUA YA 278: Jiulize Swali Hili Kama Hujajua cha Kufanya.
Inawezekana umefika sehemu unaona kwamba haiwezekani kabisa. Umeanza kuona hali uliyonayo ndio ulitakiwa hivyo. Wakati mwingine umeshaanza na kusema kwamba wewe ulizaliwa uwe maskini. Jambo moja unapaswa kujiuliza ni kwamba kama kungekuwa hakuna kushindwa, hakuna changamoto, hakuna ugumu wowote ni jambo lipi hilo ungechagua kulifanya hadi ufikie mafanikio makubwa. Ni kitu gani ungependa dunia ikutambue…
HATUA YA 277: Nenda Zaidi ya Uwezo Wako.
Kuna nyakati ili upate matokeo Zaidi ya unayopata sasa hivi utapaswa kufanya vitu ambavyo hujawahi kufanya, utatakiwa kuongea na watu ambao hujawahi au hujazoea kuongea nao. Hapo unakuwa umesogea mbele Zaidi ya uzio ambao ulikuwa umejiwekea. Lazima utaanza kuona matokeo ya tofauti na uzoefu wa tofauti pia. Kuna hali zipo kwenye biashara zetu, mahusiano na…
HATUA YA 276: Umejitoa Kwenye Nini?
Umejitoa kwenye nini? Vitu gani unafanya kila siku na unatarajia kufikia makubwa miaka michache ijayo? Malengo yako yanahusu nini Zaidi? Vipaumbele vyako vimegusa kwa vile vitu ulivyochagua kuwa navyo au unavyotaka vitokee kwenye maisha yako? Kama mpaka sasa hakuna jambo ambalo umejitoa kwa ajili ya hilo basi unapoteza muda na maisha yako. Huwezi kusema maisha…
HATUA YA 275: Kuna Tumaini.
Pamoja na mambo magumu unayopitia kwenye maisha yako kukataliwa, kuachwa, kusemwa vibaya tambua kwamba bado lipo Tumaini. Unapoona giza limeongezeka ujue kunakaribia kuwa asubuhi. Kuna hadithi yako inatengenezwa kwa hayo unayopitia. Ipo siku utasimama na kutoa ushuhuda wa maisha uliyopitia. Ona magumu yako kama shule ya kukufikisha sehemu kuu Zaidi. Hakuna mtu mkuu ambaye hajapitia…
HATUA YA 274: Unaufahamu Udhaifu Wako?
Kila binadamu kuna sehemu ambayo inakuwa ni rahisi sana kwake kufanya makosa hasa inapotokea ameingia katika mtego. Haiwezekani hata siku moja ukafikia ukuu kwenye kile unachokifanya kama huujui udhaifu wako. Hakuna binadamu ambaye hajawahi kufanya makosa yaani nikiwa na maana kwenye kile unachokifanya kuna kitu ambacho kinakuwa sababu ya wewe kushindwa mara kwa mara. Ukiona…