464; USIISHIENJIANI LEO : Kuwa Glasi Tupu.

Kati ya glasi iliyo tupu na iliyojaa maji siku zote ile tupu ndio hupata nafasi ya kuwekewa maji mengine.

Watu wengi tunapenda Kuonekana tunajua kila kitu. Tunapenda Kuonekana sisi kuliko hata vile tunavyovifanya.

Ni muhimu ujue kuwa Unapokuwa kama glas tupu maana yake wewe ni mtu unaefanyia kazi yale ujifunzayo.

Huachi glasi ikiwa na maji bali unachukua hatua na kiu yako ya kutaka kujifunza inaongezeka.

Yafanyie kazi yale unayojifunza. Hujifunzi ili uje uoneshe wengine wewe unajua kuliko wao.

Unapokuwa Glasi iliyotupu unajiweka katika utayari wa kupokea vitu Vipya ndani yako.

Nakutakia Kila la Kheri.
Ubarikiwe sana.
Rafiki Yako Jacob Mushi.
jacobmushi.co.tz/huduma

Get new articles

I’ll send you new articles as soon as they come out — by email, WhatsApp, or both.

Fill in either one, or both.

Toa maoni yako

Barua pepe yako haitaonyeshwa.

Chukua hatua moja leo.

Kila kitabu nilichoandika kimezaliwa kutoka makala kama hii. Kama kuna unachotaka kunieleza, niandikie.

Jiunge Nunua Kitabu