Mwaka 2016/17 nikiwa Arusha, mimi na rafiki yangu tulipata wazo kubwa: kutengeneza app au mfumo wa kusaidia watu kukata tiketi za mabasi mtandaoni, mkoa kwa mkoa. Tulikaa kwenye hoteli maarufu Palace Hotel, tukapanga kila kitu kwa kina, na kuandika yote kwenye notebook ambayo bado ninayo hadi leo.
Tulianza hatua za awali: kutafuta takwimu za idadi ya mabasi, safari, na idadi ya wasafiri wa kila siku. Tulihitaji data ili kuunganisha mfumo wetu na kampuni za mabasi. Lakini hatukufaulu kupata taarifa hizo, na hatimaye tulikwama.
Miaka michache baadaye, mwaka 2018, nikahamia Dar es Salaam na kuendelea na huduma za IT chini ya kampuni yetu, Moja Technologies, ambayo leo inajulikana kama Netpoa.
Siku moja, niliona app mpya ikijulikana kama BusBora, ikifanya kile tulichowaza miaka kadhaa nyuma. Nikaitumia mara kadhaa kukata tiketi, na kila mara nikitumia nikajisikia kuwa: “Hili ndilo tulilowaza pale Arusha.”
Hapa ndipo pale nilipojifunza somo muhimu la maisha na biashara:
Wazo lolote linalokuja akilini mwako ni sehemu ya mafanikio yako. Lakini kama hutachukua hatua, wengine watachukua hatua hiyo na kufanikiwa.
Wazo bila utekelezaji ni ndoto tu. Kila wazo linahitaji ujasiri wa kuanza, hata kama huna kila kitu mkononi. Ukianza, hatua ndogo ndogo zinakusogeza mbele, na dunia huanza kukusaidia.
Kwa hivyo, kama unazo ndoto au wazo, usisubiri hadi kila kitu kiwe kamili. Chukua hatua sasa. Andika, panga, jaribu, hata ukikosa mara ya kwanza. Hii ndiyo njia pekee ya kuona wazo lako likitokea halisi.
Unaweza pia kununua kitabu changu cha Usiishie Njiani na kuona jinsi unavyoweza kuendelea kusonga mbele licha ya changamoto: [Nunua Kitabu Hapa].
Discover more from Jacob Mushi
Subscribe to get the latest posts sent to your email.

